Home Kimataifa BAADA YA MSIMU BORA ULIOPITA, ATLANTA HAWKS WAANGUKIA KIDEVU KWA DETROIT

BAADA YA MSIMU BORA ULIOPITA, ATLANTA HAWKS WAANGUKIA KIDEVU KWA DETROIT

512
0
SHARE
Stan Van Gundy kocha wa Detroit katika moja ya ushangiliaji wake
Stan Van Gundy kocha wa Detroit katika moja ya ushangiliaji wake

Kocha wa Atlanta Hawks, Mike Budenholzer ilibidi akubali tu kuwa timu yake haikufanya vyema usiku wa jana baada ya kuzidiwa kwa kila namna na timu ya Detroit Pistons. Ilikuwa ni ngumu kuamini kama hii ndio Atlanta Hawks iliyoshinda michezo 60 na kupoteza 22 peke yake msimu uliomalizika na kuongoza kanda ya mashariki.

Kocha wa Detroit Pistons Stan Van Gundy hakusita kuisifu timu yake kwa kuweza kudaka rebound nyingi sana kiasi cha kuwapa ushindi ijapokuwa walikuwa na shabaha ya asilimia 38.5, yaani mitupo 37 tu kati ya 96 waliyojaribu.

Kentavious Caldwell-Pope aliwaongoza wenzake wengine walioanza  wa Detroit katika kufunga pointi zenye tarakimu mbili kila mmoja akifunga pointi 21, Reggie Jackson akifunga 15, Marcus Morris alifunga 18 akidaka rebound 10, Andre Drummond alimaliza na point 18 huku akidaka rebound 19 mapema kabisa katika mchezo huo, Ersan Ilyasova yeye akifunga pointi 16.

Mjerumani Dennis Schroder yeye aliwaongoza Atlanta Hawks na pointi 20, Paul Millsap akafunga 19, Jeff Teague akafunga 18, huku mchezaji mpya aliyechukua nafasi ya Demarre Carroll, anayeitwa Kent Bazemore yeye akimaliza bila kufunga pointi yoyote.

Paul Millsap yeye alikaririwa akisema watarejea katika ubora wao mapema zaidi ya inavyodhaniwa na kuwa hawakuwa vizuri katika mchezo huu.

HIGLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here