Home Kimataifa NANI KUTWAA MVP KATIKA NBA? HUU NI UTABIRI WANGU NA WA WACHAMBUZI...

NANI KUTWAA MVP KATIKA NBA? HUU NI UTABIRI WANGU NA WA WACHAMBUZI MBALIMBALI ULIMWENGUNI

725
0
SHARE

Na Nicasius N Agwanda (Nicasius Coutinho Suso)

Kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuanza rasmi alfajiri ya kuamkia kesho, kumekuwa na tabiri tofauti kuhusiana na nani anaweza kuwa MVP au mchezaji mwenye thamani zaidi kwa msimu ujao, ikumbukwe kuwa msimu uliomalizika tuzo hii ya heshima ilikwenda kwa mchezaji wa klabu ya Golden State warriors Stephen Curry. Nani atatwaa msimu huu?

ANTHONY DAVIS

Anthony Davis
Anthony Davis

Kwangu huyu ndiye mchezaji bora zaidi kwa sasa ukiachana na Lebron James na aliyekamilika. ni mchezaji anayekupa vitu vingi ndani ya uwanja kuanzia ukabaji, ambapo mikono yake mirefu imekuwa msaada mkubwa kwake katika kupokea Rebounds, kupiga blocks, na kama hiyo haitoshi wastani wake wa pointi unaridhisha akiwa na zaidi ya asilimia 50% jambo pekee ambalo halikuwa halijaonekana sana kwake ni utupaji wa pointi tatu, na katika mechi za majaribio inaonekana kalifanyia kazi sana. ikumbukwe huyu ndiye mchezaji aliyekuwa na wastani mzuri wa ufanisi (Players Effeciency Ratio (PER). hivyo kama New Orleans Pelicans watafika walau nafasi ya tano au sita nampa sana nafasi. timu yake iepuke majeruhi na yeye akae fiti maana ni mtu anayeumia mara kwa mara.

LEBRON JAMES

Lebron James akipokea moja ya tuzo zake za MVP wa NBA
Lebron James akipokea moja ya tuzo zake za MVP wa NBA

Wazungu wanasema he’s arguably the best. ndio ni mchezaji bora sana, lakini MVP haihesabu ubora wako wa muda wote bali ni namna msimu ulivyokuijia. napenda namna anavyokuwa na wastani mzuri wa pointi, assist, na rebound. na ukizingatia timu yake ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa mashariki kuna kila uwezekano wa yeye kuwa na MVP nyingine tena msimu. ana bahati mbaya tu ya kushinda fainali anazofika lakini ni mchezaji bora na moja ya wachezaji bora wa muda wote. ukiamua kumlinganisha na Michael Jordan nayo sawa lakini uwe umejiandaa.

STEPHEN CURRY

Stephen Curry baada ya kupokea tuzo ya MVP wa ligi msimu wa 2014/15
Stephen Curry baada ya kupokea tuzo ya MVP wa ligi msimu wa 2014/15

Usitegemee kama Golden State warriors watacheza mbali sana msimu huu hata kama wasipoongoza kanda yao. akiwa ni mchezaji anayeonekana kuja kuwa bora kwa muda wote katika urushaji wa point tatu, Stephen Curry anabaki kuwa mchezaji bora sana, na anayebebwa na namna timu yake inavyocheza. msimu uliomalizika alikuwa ni mchezaji aliyefunga pointi nyingi zaidi huku akicheza dakika chache, na kutokana na tinu yake kustukiza msimu uliomalizika msimu huu hautokuwa rahisi kwao hivyo Draymond Green, Klay Thompson na Iguodala nao wanatakiwa wacheze kama wanahitaji hiyo tuzo hili kumpunguzia mzigo. ni ngumu sana kutwaa tuzo hiyo mfululizo na haitokuwa rahisi msimu ila anaweza kuchukua.

JAMES HARDEN

James Harden akirusha Free Throw
James Harden akirusha Free Throw

Yeye Mwenyewe na wachezaji wengi wanaamini kuwa alitakiwa kuchukua tuzo hii msimu uliomalizika. ndio ana kila sababu ya kuamini hivyo, aliibeba Houston iliyokuwa inakumbwa na majeruhi chungu nzima kuanzia akina Howard mpaka Patrick Berveley, lakini hakubahatika kushinda hivyo kuishia nafasi ya pili. msimu huu atapata msaada mkubwa kutoka kwa mchezaji mpya Ty Lawson aliyetoka Denver Nuggets ambaye atampunguzia majukumu. tegemea msimu mgumu sana kipindi hiki pengine kuliko msimu uliopita, na kama akicheza kwa kiwango kile anaweza kufanya makubwa, na ikawa kipozeo baada ya kuachwa na Khloe Kardashian.

Kevin Durant

Kevin Durant akipokea tuzo ya MVP wa NBA msimu wa 2013/14
Kevin Durant akipokea tuzo ya MVP wa NBA msimu wa 2013/14

hii ndio nafasi ambayo imenipa wakati mgumu sana wa nani nimuweke kati ya wachezaji wawili wa timu moja, Kevin Durant au Russell Westbrook. msimu uliomalizika Durant alikumbwa na majeraha yaliyomweka nje msimu mzima, na Westbrook akaonyesha ukomavu wa aina ya kipekee kuweza kuibeba Oklahoma City Thunders timu ya zamani ya Hasheem Thabeet hii mpaka katika nafasi ya 9 na almanusura awaingize katika raundi ya mtoano. Lakini ukweli unabaki kuwa Durant ndiye mchezaji bora wa klabu hiyo na hakuna uwezekano mkubwa wa timu kuejngwa nje yake huku kimahesabu akiwa ndiye mchezaji bora wa pili katika ligi kwa sasa nyuma ya Knga James. Akiepuka majeruhi atakuwa moja ya wanaoshindania tuzo hii.

 

RUSSELL WESTBROOK

Rusell Westbrook alivyoshinda tuzo ya MVP All Star Game
Rusell Westbrook alivyoshinda tuzo ya MVP All Star Game

Nia yangu ilikuwa nitoe majina matano tu lakini mchezaji huyu ana kila sababu ya kuongezwa hapa. Aliibuka ghafla na kufunga point nyingi huku akijichukulia jina la TRIPLE DOUBLE THREAT yaani alikuwa anapata zaidi ya tarakimu mbili katika nyanja tatu tofauti lakini mara nyingi ikiwa ni point, rebound na assist. Aliuchukua ubora huu na kwenda kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi katika mechi ya mastaa (NBA ALL STAR) hivyo ana kila sababu ya kuwepo hapa. Lakini kama nilivyosema hapo kwa Durant huyu atategemea sana kama Durant ndiye timu itamzunguka lakini ni mara nyingi tu ameweza kufunga pointi nyingi hata Durant akiwepo ila hakuwa amepewa jicho la kumtizama,ila msimu huu ataangaliwa.

WANAOWEZA KUSHANGAZA NA KUCHUKUA

  • Lamarcus Aldridge, kama atairejesha juu sana San Antonio
  • Blake Griffin, awe katika ubora wa kuiweka juu Los Angeles Clippers
  • Chris Paul, naye kama Griffin tu (wapo timu moja)
  • Paul George, hazungumzwi sana lakini ni mchezaji mzuri na kama Indiana Pacers itarudi juu basi mtizame huyu

HII VIDEO NI WACHAMBUZI WA MTANDAO WA BLEACHER REPORT, WASIKILIZE UTABIRI WAO.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here