Home Kitaifa MWADUI FC Vs YANGA…MECHI KALI YA MASTAA WAZAWA Vs MAPROO

MWADUI FC Vs YANGA…MECHI KALI YA MASTAA WAZAWA Vs MAPROO

838
2
SHARE

DFDSDFZGXB

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC watakuwa wageni wa Mwadui FC katika mchezo wa raundi ya 8 na 9 siku ya Jumatano hii katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga. Timu hizo zinakutana kwa mara ya kwanza katika ligi kuu na licha ya kupanda msimu huu Madui chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘ Julio’ imekuwa ikitazamwa na wadau wengi wa kandanda nchini kutokana na timu hiyo kuwakusanya wachezaji wengi wenye majina makubwa Tanzania hususani wale waliowahi kuzichezea klabu za Simba na Yanga.

Julio na kikosi cha Mastaa Mwadui FC…..
Mwadui FC itakuwa na mlinda mlango bora wa msimu uliopita Shaaban Kado tayari imeruhusu magoli Manne katika mechi 8 ilizokwisha cheza. Ikiwa katika nafasi ya Tano ya msimamo nyuma ya vinara Yanga kwa alama 5 kikosi cha Julio kinaweza kuisumbua sana Yanga kwa kuwa kitakuwa na wachezaji wasiopungua 6 ambao wamewahi kuichezea Yanga kwa nyakati tofauti.

Kado, Athumani Idd ‘ Chuji’, Nizar & Razaq Khalfan, David Luhende na straika Jerry Tegete ni wachezaji ambao wamewahi kuichezea Yanga na kushinda mataji kadhaa ya ligi kuu. Si hao tu, Mwadui FC ina wachezaji wazoefu kama nahodha wa timu, Jabir Aziz ‘ Stima’ ambaye ni mchezaji mshindi wa ligi kuu akiwa na klabu za Simba SC na Azam FC, Malika Ndeule mlinzi wa kulia wa zamani wa Azam FC. Hawa ni baadhi tu ya wachezaji ambao si wa kubeza.

Mwadui imefanikiwa kushinda gemu nne kati ya 8 walizocheza. Wamepoteza gemu mbili ( dhidi ya Toto Africans, CCM Kirumba, na dhidi ya Azam FC, Mwadui Complex). Kiuchezaji bado Julio anatafuta uwiano ulio sawa kwa kuwa baadhi ya wachezaji wake wamekuwa wakikubwa na majeraha ya mara kwa mara. Rashid Mandawa, mshambulizi huyu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars bado ameshindwa kufikia kiwango chake cha ufungaji cha msimu uliopita.
Mandawa alifunga zaidi ya magoli 11 akiwa Kagera Sugar lakini hadi sasa kufikia mechi ya 8 katika timu ya Mwadui FC hali si nzuri. Paul Nonga pia bado hajafikia ubora wake ule aliouonesha akiwa na timu ya Mbeya City FC katika misimu miwili iliyopita lakini kwa kiwango cha washambuaji wa daraja la juu Tanzania bila shaka Julio ana machaguo matatu makini, Tegete, Mandawa na Paul ambao wanaweza kuisaidia timu yao kuishinda Yanga.
Mwadui FC wanaweza kuwazuia Yanga wasifunge kwa mara ya kwanza msimu huu?
Yanga wamefunga magoli 18 ( magoli 10 zaidi ya Mwadui FC) imekwenda Shinyanga ikiwa na kikosi kamili licha ya mlinzi wa kati Kelvin Yondan kushindwa kumaliza gemu ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Toto Africans wiki iliyopita. Safu ya mashambulizi ya Yanga chini ya washambuaji Mzimbabwe, Donald Ngoma, Mrundi, Amis Tambwe na mfungaji bora wa msimu uliopita Saimon Msuva imeonekana kuwa hatari zaidi kwa beki za timu pinzani hadsi sasa.

Watatu hao wamefunga jumla ya magoli 13 kwa timu yao. Tambwe na Ngoma kila mmoja amefunga mara tano wakati Msuva aliyefunga mara mbili katika mechi iliyopita amefikisha magoli matatu. Yanga itaendelea kuwategemea zaidi washambuaji hao huku nyongeza na Malimi Busungu ikitaraji kuendelea kuwabeba katika gemu ngumu.

Mwadui FC wana safu ya ulinzi yenye uzoefu, pia kiujumla wana timu yenye wachezaji waliopevuka kiumri na kimpira. Ndeule, Luhende, Kado, Anthony Matogolo, Malegesi Mwangwa ni baadhi ya walinzi ambao Julio anataraji kuwatumia kuhakikisha Yanga hawafungi kwa mara ya kwanza msimu huu. Kikosi cha Muholanzi, Hans Van der Pluijm kimefanikiwa kufunga katika kila mchezo huku safu yao ya ulinzi ikiruhusu magoli matatu tu katika mechi 7 walizocheza.
Itakuwa mechi kali kwa hakika kwa kuwa hata Madui imekuwa na wachezaji wazuri. Razaq, Jabir, Suleimani Kassim, Jabir wanaweza kucheza bila hofu katika safu ya kiungo. Hans anaweza kuwapanga Thaban Kamusoko, Salum Telela na Haruna Niyonzima katika safu ya kati ili kuwadhibiti Mwadui FC ambao waliibana sana Azam FC wiki nne zilizopita.

Timu zote ‘ wagonjwa’ wa penalty………
Timu zote zimekuwa na bahati ya kupata mikwaju ya penalty. Yanga wamepoteza mara mbili mfululizo mikwaju ya penalty. Kamusoko alikosa katika gemu ya sare ya kufungana 1-1 na Azam FC wakati Ngoma alishindwa kufunga dhidi ya Toto. Kwa upande wa Mwadui FC, Nizar aliweka rekodi ya mchezaji wa kwanza aliyepoteza mkwaju wa penalty katika ligi kuu msimu huu. Alishindwa kufunga dhidi ya Toto siku ya ufunguzi wa msimu kisha Mandawa akashindwa pia kufunga katika gemu dhidi ya Azam FC.

Safu ya Mashambulizi ya Mwadui FC vs Safu ya ulinzi ya Yanga SC
Tegete amefanikiwa kuifungia Mwadui magoli matatu katika mechi tatu alizoichezea timu hiyo msimu huu. Mshambuaji huyu wa zamani wa Taifa Stars amejiunga na Mwadui baada ya kuichezea Yanga tangu msimu wa 2008/09. Aliachwa kwa sababu za kushuka kwa kiwango chake lakini si ajabu akaibuka shujaa ya gemu hii kama tu walinzi wa Yanga, Kelvin na nahodha, Nadir Haroub hawatakuwa makini.
Itapenda sana kama Julio atawapanga washambuaji wake watatu kwa sababu itasaidia kuwafanya walinzi wa pembeni wa Yanga kushindwa kupanda mara kwa mara kwa kuhofia kufungwa. Paul, Mandawa na Tegete itakuwa safu kali ya mashambulizi ambayo inaweza kuwasaidia Mwadui kushinda mechi hii. Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji wanaweza kuanza katika fullbacks za Yanga na wawili hawa wamekuwa wakichangia sehemu kubwa ya magoli ya timu yao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here