Home Kitaifa MGOSI AWATIA MOYO WAPENZI WA SIMBA

MGOSI AWATIA MOYO WAPENZI WA SIMBA

706
0
SHARE
Mussa Hassan Mgosi nahodha wa kikosi cha Simba SC
Mussa Hassan Mgosi nahodha wa kikosi cha Simba SC
Mussa Hassan Mgosi nahodha wa kikosi cha Simba SC

Mchezaji mkongwe na nahodha wa klabu ya Simba SC Musa Hassan Mgosi amewataka wapenzi wa Simba kutokata tamaa kutokana na matokeo ya kufungwa mechi mbili hadi sasa kati ya mechi nane walizocheza tangu kuanza kwa ligi msimu huu.

Mgosi amesema, bado ni mapema kwa mashabi wa Simba kukataa tamaa na timu yao kwani bado kuna mechi nyingi za kucheza ambazo timu ya Simba inaweza kupata matokeo mazuri na kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom mimu huu.

“Kwa upande wangu mimi sijaona sababu ya wao kukata tamaa kwasababu ligi ndio kwanza sasahivi mechi ya nane na ukiangalia kwenye suala la mpira hata hao Yanga waliokua mabingwa msimu uliopita, walipoteza mechi nne au tano kama sikosei, lakini mwisho wa siku wakachukua ubingwa”amsema Mgosi.

“Kupoteza mechi mbili kati ya nane kwenye ligi sio suala la kukata tamaa kikubwa ni kwamba sisi wenyewe tumejiwekea malengo ya kupata ubingwa au tufanye kile ambacho wapenzi wa Simba wameki-miss siku nyingi”.

“Kwa maana hiyo sasa, haijalishi kufungwa na Tanzania Prisons na Yanga basi yale malengo yakawa yamepotea kwetu sisi na kile ambacho tunakitaka kikawa kimepotea hapana. Hata ukiangalia ligi za Ulaya Barcelona wanafungwa lakini mwisho wa siku wao ndio wanakua mabingwa”.

“Kwahiyo nawaambia mashabiki wa Simba yale yaliyotokea tuyaweke pembeni tuangalie ni umoja gani na changamoto tunazozipata sisi kwenye kupata matokeo, hayo ambayo tumeyapata Mbeya ni changamoto kwetu sisi kuangalia makosa yako wapi na tukayarekebisha ili katika mechi ya kesho tufanye vizuri”.

“Huwezi kujua hizo timu ambazo zinashinda kwasabu kwa Tanzania Simba na Yanga ndio timu ambazo zinaangaliwa, kwa hiyo hapo wapenzi wa Simba wanaangalia Yanga wamepata matokeo gani na mashabiki wa Yanga wanaangalia Simba wamepata matokeo gani”.

“Lakini wakumbuke hao Yanga wana mechi ya nane lakini wametoka nje mechi moja tu na inafahamika mechi za nje kuna changamoto zake kama uwanja na changamoto nyingine ambazo zinajulikana. Katika mechi zetu nne ambazo tumetoka nje tumefanikiwa kushinda mechi tatu”.

“Kufungwa kwetu tusianze kumtafuta mchawi nani, tuangalie matatizo yapo wapi na makosa yako wapi. Kikubwa kwa wapenzi wa Simba wasikate tamaa na nafikiria malengo ambayo tumejiwekea, bado mapema sana naamini matokeo yatapatikana kwasabu timu ni nzuri”.

“Kwa matokeo tuliyopata kwenye mechi ya Mbeya dhidi ya Prisons, kila mchezaji mwenye akili timamu na mwenye kutaka maendeleo na amani naamini kwenye mechi ya kesho tufanye kile ambacho wana Simba wanakitaka”.

Simba itakutana na Coasta Union kwenye mchezo wake wa kesho wa ligi kwenye dimba la taifa huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Tanzania Prisons ikiwa ugenini kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here