Home Kitaifa KOCHA WA ZAMANI WA TANZANIA PRISONS KUFANYIWA UPASUAJI WA KICHWA

KOCHA WA ZAMANI WA TANZANIA PRISONS KUFANYIWA UPASUAJI WA KICHWA

571
0
SHARE
Kocha wa zamani Tanzania Prisons David Mwamaja
Kocha wa zamani Tanzania Prisons David Mwamaja
Kocha wa zamani Tanzania Prisons David Mwamaja

Kocha wa zamani wa timu ya Tanzania Prisons ya Mbeya David Mwamaja, amelazwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya kuanguka iliyosababisha kuumia kichwa pamoja na mbavu.

Kwa mujibu wa binamu wa Mwamaja Bw. Boaz Ikupilika, Mwamaja anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa kwa kile kinachodaiwa huenda damu ikawa imevilia kichwani hivyo upasuaji itakuwa ni njia pekee ya kutatua tatizo hilo linalo mkabili kocha huyo.

“Alipata ajali ya kuanguka akaumia mbavu na kichwa, alijigonga kichwa, baada ya kujigonga kichwa akaenda hospitali na kupatiwa huduma za awali akajisikia yuko vizuri. Baada ya muda akawa hajisikii vizuri lakini walikuwa wanasafiri na timu kweda Mbeya walikuwa na mechi dhidi ya Kimondo”, amesema Ikupilika.

“Akiwa Mbeya ndiko hali ilianza kumbadilikia akarudi hadi hospitali ya wilaya ya hapo Njombe ambapo alipata matibabu, ilikuwa tare 21 mwezi huu baada ya matibabu ya pale akahamishiwa Mhuhimbili ilikuwa tarehe 23”.

“Ajali alipata kama wiki tatu zilizopita, baada ya kupata ajali akaendelelea na mazoezi na kazi zake kama unavyojua ni mtu wa mazoezi lakini madhara yalianza kuonekana kuanzia tarehe 18 na 19 wakati wanacheza na hiyo timu ya Kimondo. Leo ameanzishiwa tiba na dawa ameandikiwa na vipimo”.

“Siwezi kusema kwamba anaendelea vizuri kwasababu kwa mujibu wa maelezo ya daktari, bado hajatengemaa anahitaji upasuaji wa kichwa kwasababu kunauwezekano kwamba damu imevilia kichwani”.

“Kikubwa ambacho anahitaji sasahivi ni kuweza kupatiwa matibabu kamili ambayo yatatokana na kufanyiwa upasuaji wa hapa Muhimbili (MOI), pia anatakiwa kufanyiwa vipimo vya awali kabla ya upasuaji ambavyo ndio tuhangaika navyo mpaka sasa na dawa ambazo ameandikiwa ni dawa za gharama kutokana na aina ya ugonjwa uliogundulika kwake”.

“Tunahitaji wadau wamsaidie kwasababu inaonekana hata alipotoka kule hakupata msaada stahiki kwa wakati kutokana na alikuwa na madeni na hiyo klabu walikuwa bado hawajamkamilishia malipo yake kwahiyo bado hata kiuchumi hakuwa vizuri”.

Mwamaja alikuwa anakinoa kikosi cha Tanzania Prisons kinachoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kabla ya kutimuliwa raundi ya pili msimu uliopita baaya kikosi hicho kufanya vibaya kwenye michezo yake na kuwa nafasi ya mwisho kwa muda mrefu kabla ya Mbwana Makatta kukinusuru kikosi hicho kisiteremke daraja alipochukua nafasi ya Mwamaja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here