Home Kitaifa KERR AMEPEWA MECHI 2 SIMBA SC, STRAIKA WATAMUANGUSHA?

KERR AMEPEWA MECHI 2 SIMBA SC, STRAIKA WATAMUANGUSHA?

761
1
SHARE

 

DFSGFDHNNa Baraka Mbolembole, Dar es Salaam

Vipigo viwili katika mechi 7 za ligi kuu tayari zimewafanya viongozi wa klabu ya Simba SC kumpatia mechi mbili kocha wao raia wa Malta, Dylan Kerr kabla ya kufikia uamuzi wa kumfuta kazi kocha huyo Muingereza. Kiasi hata, Kerr mwenyewe ameshangazwa na uamuzi huo lakini kwa namna yoyote anapaswa kufanya vizuri zaidi kuanzia gemu ya Jumatano hii dhidi yo Coastal Union katika uwanja wa Taifa.
Simba haichezi vile ilivyotarajiwa na kitendo cha kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Tanzania Prisons kimefanya wapenzi na baadhi ya mashabiki wa timu kuanza kuhoji uchezaji wa timu yao. Simba haichezi vizuri, mbinu za ufungaji si za kuvutia. Kwa kiasi kikubwa safu ya ulinzi ya timu hiyo ndiyo imechangia kwa kiasi kikubwa mwanzo mzuri kiasi wa timu hiyo msimu huu.

Ikiwa na alama 15 kikosi cha Kerry kipo nafasi ya tano nyuma ya vinara Yanga SC, Azam FC kwa pointi 4, wamepitwa alama moja na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 3 huku wakifungana pointi na Stand United iliyo nafasi.

Kerr amesema kuwa hakuna kipengele cha kumfuta kazi katika mkataba wake wa Simba lakini ni mara chache sana Simba imekuwa na uvumilivu kwa makocha ambao hushindwa kufanya vizuri. Muingereza huyo alipewa nafasi kubwa ya kuwatathimini wachezaji mbalimbali wakati wa usajili na ni yeye aliyependekeza kusainiwa kwa mshambuaji Pape N’daw raia wa Senegal .

Kerr hakuonekana kung’ang’ania usajili wa mshambuaji Kelvin Ndayisenga raia wa Burundi ambaye kwa kiasi kikubwa angifanya safu ya ushambuaji ya Simba kuwa na makali akicheza sambamba na Mganda, Hamis Kiiza ambaye ameifungia Simba magoli matano katika gemu tatu tu alizoichezea timu hiyo katika ligi kuu.

Kumpa mechi mbili za kutazama uwezo wa Kerr ni jambo zuri kwa uongozi kwa sababu wanaonekana kutolizishwa na kiwango cha timu kiuchezaji. Simba haina matokeo ya kuwafanya wamfute kazi Kerr lakini wanaweza kufanya hivyo kama timu yao itapoteza mechi mbili zijazo kwa sababu endapo Yanga na Azam wataendelea kushinda katika gemu mbili zijazo na Simba wakashindwa kufanya hivyo watajikuta wameachwa kati ya alama 8-10 wakati ligi ikiwa katika mzunguko wa Nane tu.

Kumpa gemu mbili Kerr kutachochea tena uwajibikaji katika benchi la ufundi ambalo linawajibika kuifanya timu hiyo kucheza vizuri na kupata matokeo. Katika ligi ya msimu huu kupoteza gemu nne tu inakufanya kuwa nyuma sana kwa pointi. Simba wanahitaji kushinda zaidi kwa sababu malengo yao ni kumaliza ndani ya nafasi 2 za juu.

Mchezo dhidi ya Coastal Jumatano hii ni mgumu sana kwa kuwa timu hiyo ya Tanga haijapoteza dhidi ya Simba katika gemu 6 mfululizo za ligi kuu. Coastal wameshindwa kumpilipa kocha raia wa Uganda, Jackson Mayanja ndiyo maana mkufunzi huyo ataendelea kuisimamia timu hiyo licha ya kutangazwa kufutwa kazi wiki iliyopita.

Licha ya kufanya vibaya msimu huu, Coastal inaweza kumuharibia zaidi Kerr kama mkufunzi huyo wa Simba ataendelea kutatua tatizo la ufungaji katika timu yake. Simba imefunga mara Nane tu katika gemu 7 za ligi kuu nan i mchezaji mmoja tu wa safu ya mashambulizi aliyekwishafunga ( Kiiza).

Coastal wamefanikiwa kufunga goli moja tu na wala haionekani kama timu tishio mbele ya Simba. Mechi hii huenda ikawa sare-tasa kwa kuwa timu zote hazina wafungaji mahiri. Simba si tishio kwa kuwa haina safu kali ya mashambulizi. Coastal ni ‘ butu’ kabisa. Makipa watakuwa na mechi rahisi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here