Home Kimataifa CRISTIANO RONALDO KUCHEZA TENA NA WAYNE ROONEY.

CRISTIANO RONALDO KUCHEZA TENA NA WAYNE ROONEY.

691
0
SHARE

roobte

Wayne Rooney na CR7 ni marafiki wa karibu sana hadi sasa hivi licha ya kucheza club tofauti na kupitia mambo mengi kwenye mchezo wa soka.

Sasa kuna uwezekano mkubwa ambapo Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo watacheza tena pamoja kwenye mechi maalum kwa ajili ya Rooney. Manchester united imethibitisha kwamba kutakuwa na mechi maalum kwa ajili ya kutambua miaka 12 aliyocheza Rooney ndani ya Old Trafford.

Mechi hiyo ambayo itafanyika kwenye uwanja wa Old Trafford itakua dhidi ya Everton ambayo ni club ya zamani ya Rooney kabla hajahamia United.

Rooney anategemea kuwaalika marafiki zake wakaribu ambao amecheza nao au hajawai kucheza noa soka kwenye hiyo mechi kwa ajili yake. Kuna uwezekano mkubwa CR7 akaja kucheza mechi ya heshima kwa ajili ya rafiki yake.

Pia kila pesa itakayopatikana kwenye mechi hiyo zitatumika kwa ajili ya kujitolea kwenye mambo mbalimbali. Mechi hiyo itafanyika mwakani kwenye muda wa mechi za pre-season

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here