Home Kimataifa CHRIS SMALLING MIONGONI MWA WALINZI 3 BORA DUNIANI

CHRIS SMALLING MIONGONI MWA WALINZI 3 BORA DUNIANI

716
0
SHARE

Chris Smalling 2Beki wa Manchester United Chris Smalling anatajwa kuwa miongoni mwa walinzi watatu bora wa kati hivi sasa duniani. Kauli iliyotoka kwa nahodha wake wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Wayne Rooney.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu wa Manchester United, alipoulizwa kuhusu uwezo wa Chris Smalling msimu huu, Rooney amesema, anakubali kupanda kwa kiwango cha mlinzi huyo msimu huu huku akimtaka aendelee kuwa kiongozi katika safu ya ulinzi.

Rooney anasema, “Chris ni miongoni mwa mabeki wakati bora hivi sasa. Ni miongoni mwa mabeki bora watatu wakati hivi sasa duniani”.

Tayari wiki kadhaa nyuma, kocha Louis Van Gaal alimwagia sifa Chris Smalling kwakua na uwezo mkubwa kikosini hivi sasa, huku akimtaka siku moja kuchukua mikoba ya unahodha wa Manchester United baada ya Rooney na Carrick kuondoka.

Smalling anatajwa kuwa ndiye mchezaji aliye-perform katika kiwango cha juu msimu huu katika kikosi cha Louis Van Gaal, na kwamba ndiye mchezaji bora wa klabu tangu kuanza kwa msimu.

Aidha Rooney alimwagia pia sifa kijana chipukizi Anthony Martial aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Monaco kwamba ni miongoni mwa wachezaji muhimu kikosini hivi sasa na kwamba atawasaidia kupata chochote msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here