Home Kimataifa TANZIA KWA WADAU WA LIGI YA NBA

TANZIA KWA WADAU WA LIGI YA NBA

699
0
SHARE

DFD

Kocha na Rais/mkurugenzi wa mambo ya ufundi katika klabu ya Minnesota Timberwolves, Flip Sounders amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 60, kubwa likisemekana ni ugonjwa wa kansa ( Hodgkin’s lymphoma)  uliokuwa ukimsumbua muda mrefu sasa. Sounders alilazwa tangu mwezi septemba na kafariki Jumapili hii, na hili linakuwa pigo kwa wapenzi wa NBA hasa klabu ya Minnesota Timberwolves kutokana na mchango alioutoa klabuni hapo kwa muda mrefu sasa, na tukiwa tunaelekea katika msimu mpya wa NBA utakaoanza tarehe 27 siku ya Jumanne

Katika kipindi cha miaka 35 ya ukocha wake Saunders kapata ushindi zaidi ya mara 1000, akiwa amefundisha vilabu vya Minnesota, Detroit Pistons na Washington Wizards.

Saunders alitangaza mwezi wa nane kuwa alikuwa katika matibabu maalumu ya ugonjwa wa Hodgkin’s Lymphoma. Madaktari mwanzo walihisi kuwa ulikuwa ugonjwa unaotibika na unaopona, na Saunders alikaririwa muda ule kuwa atabaki kuwa kocha wa klabu yake na Rais wa mambo ya Ufundi klabuni hapo. Lakini kutokana na khali yake kuendelea kuwa mbaya alilazwa mwezi septemba na Ijumaa ilitoka taarifa kuwa Saunders angekosa msimu mzima wa 2015-16.

Saunders alikuwa kocha wa NBA kwa mara ya kwanza mwaka 1966 akiwa na Timberwolves na akawaongoza kuingia mara nane mfululizo katika hatua ya mtoano, akiwa anasifika kama kocha anayependa aina ya ushambuliaji sana, na kuzalisha wachezaji wa kwanza yaani Point Guards lakini anakumbukwa kwa kumleta Kevin Garnett ambaye baadae alishinda tuzo ya Mchezaji bora na mwenye thamani zaidi katika ligi hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here