Home Kimataifa LAMAR ODOM BADO NJIA PANDA, KUBAKI HOSPITALI KWA MIEZI 6

LAMAR ODOM BADO NJIA PANDA, KUBAKI HOSPITALI KWA MIEZI 6

594
0
SHARE
Lamar Odom
Lamar Odom

Na Nicasius N Agwanda (Nicasius Coutinho Suso0

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Los Angeles Lakers ambayo alishinda nayo ubingwa wa NBA mara mbili na akicheza katika vilabu vya Los Angeles Clippers, Dallas Mavericks na Miami Heat khali yake imeendelea kuwa ya kuwastua wengi ingawa kuna maendeleo tofauti na awali.

Ikumbukwe kuwa Lamar Odom alikutwa katika Danguro oktoba 13 akiwa hajitambui baada ya kusekana kutumia kwa kiasi kikubwa madawa ya kulevya maarufu kwa jina la Cocaine na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume yaliyozidi kipimo.

eneo na jina la danguro alilokuwa Lamar
eneo na jina la danguro alilokuwa Lamar

Taarifa kutoka kwa rafiki yake wa karibu na kocha wake wa zamani wa chuo Jim Harrick zinasema kuwa kuna uwezekano mkubwa akabaki hospitali kwa zaidi ya miezi 6 akijaribu kupigania afya yake na kujaribu kuokolewa ili asipooze. Lamar odom amekuwa na maisha yasiyoeleweka na kukumbwa na kashifa za matumizi ya madawa ya kulevya khali iliyopelekea kuvunjika kwa ndoa yake na mwanadada wa vipindi vya Televisheni kutoka familia ya kistaa ya THE KARDASHIANS, Khloe Kardashian.

rr5

Hata hivyo tangu apate matatizo hayo Khloe amekuwa pembeni yake na baadae ikaja kuthibitika kuwa hawakufanikiwa kupata talaka yao, khali iliyopelekea Khloe kuwa bado mke halali anayetambulika na mwenye maamuzi ya kitabibu juu ya Lamar Odom. Aidha katika kuonyesha kuwa bado alikuwa anampenda sana mumewe huyu wiki iliyopita Khloe alimtuma mwanasheria wake kwenda kutengua shitaki la talaka alilokuwa ameweka, nah ii inakuja miezi kadhaa baada ya khloe kukiri kuwa hakuwahi kumsahau Lamar, na kuwa siku zote amekuwa mtu mwema kwake na kwa watu wengine.

khloe kardashiana akiwa na Lamar Odom
khloe kardashiana akiwa na Lamar Odom

Taariifa za ndani zinadai kuwa Khloe katika kipindi chote ambacho hakuwa na Lamar, alianzisha ukaribu na uhusiano uliokisiwa kuwa wa kimapenzi na mchezaji wa klabu ya Houston Rockets, James Harden ambaye pia inadaiwa hakutaka kumzuia Khloe kwenda kumuuguza mume wake huyo. Kitendo cha kuondoa talaka inasemekana litakuwa pigo kubwa kwa Harden ambaye alikuwa ameana kufall in love na mwanadada huyo.

James Harden
James Harden

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here