Home Kimataifa LAKERS YAACHANA NA JABARI BROWN YAMUINGIZA METTA WORLD PEACE

LAKERS YAACHANA NA JABARI BROWN YAMUINGIZA METTA WORLD PEACE

701
0
SHARE
Metta World Peace
Metta World Peace
Metta World Peace
jabari brown
Jabari Brown

Na Nicasius N Agwanda (Nicasius Coutinho Suso)

Sheria ya NBA inavitaka vilabu kuwa na jumla ya wachezaji wasiozidi 15 ambao wataorodheshwa kushiriki michezo ya NBA, na vilabu kadhaa msimu huu vilikuwa na idadi iliyozidi 15 hivyo kutakiwa mpaka kufikia siku ya jumatau jioni (leo hii) kuwa vimewasilisha majina ya wachezaji wanasajiliwa rasmi. Hivyo katika kutimiza masharti hayo meneja wa klabu ya Los Angeles LakersĀ  Mitch Kupchak ametoa taarifa rasmi kuwa klabu ya Los Angeles Lakers imeamua kuachana na mchezaji Jabari Brown na maana yake mchezaji mwingine aliyekuwa kwenye hatari ya kukatwa Metta WWorld Peace ambaye jina lake la kuzaliwa ni Ron Artest (alilibadili mwaka 2011 kisheria) amebaki na kikosi hicho.

Jabari brown alikuwepo katika michezo ya maandalizi na alikuwa na wastani wa pointi 6.0, Ribaundi 1.5, assist 0.8 kwa dakika 14.3 kwa kila mchezo. Katika msimu uliomalizika alicheza michezo 19 pekee huku akianza 5, na kuwa na wastani wa pointi 11.9, assist 2.1, ribaundi 1.9 kwa dakika 29.9 kwa mchezo.

ORODHA RASMI YA WACHEZAJI WA LAKERS HII HAPA

Capture

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here