Home Kimataifa KOCHA WA GOLDEN STATE WARRIORS STEVEN KERR NJE

KOCHA WA GOLDEN STATE WARRIORS STEVEN KERR NJE

539
0
SHARE

wor

Na Nicasius N Agwanda (Nicasius Coutinho Suso)

Kocha wa Golden State Warriors Steve Kerr atakosa michezo ya ufunguzi kutokana na kuendelea kupata matibabu na kupona matatizo ya mgongo aliyoyapata siku za karibuni.

Mkurugenzi wa klabu hiyo Bob Myers told katoa taarifa kuwa kocha wa muda Luke Walton ndiye ataiongoza klabu hiyo katika mchezo wake wa mwanzo dhidi ya  New Orleans Pelicans siku ya Jumanne usiku kule Oakland.  Katika hatua nyingine taarifa imetoka kuwa kocha Kerr ataudhuria tafrija ya upandishaji wa bango la ubingwa wao waliouchukua msimu uliomalizika, lakini hayupo fiti kuanza majukumu ya ukocha.

 

Kerr amekuwa na majeraha kwa muda sasa, haswa tangu kipindi cha ufunguzi rasmi wa kambi ya mazoezi ya kujiandaa na michezo ya majaribio ya NBA, na chanzo kikubwa cha kutokuwa fiti huku kikisemekana kuwa matatizo aliyoyapata wakati wa kufanyiwa upasuaji wa mgongo Julai 28. Haijajulikana bado ni lini atarudi rasmi kuendelea kuifundisha timu yake hiyo aliyoingoza kushinda taji la Nba msimu uliopita ukiwa ndio msimu wake wa kwanza akiwa kama kocha.

Katika ufunguzi wa Jumanne atakuwepo katika tafrija ya awali ambapo atapokea Pete yake, ieleweke kuwa, tofauti na michezo mingine ambayo makocha na wachezaji hupewa medali baada ya kushinda ubingwa, ligi ya kikapu NBA hutoa Pete maalumu ambazo huwa heshima ya kushinda ubingwa.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here