Home Kimataifa GERALD GREEN AKUMBANA NA FAINI YA ZAIDI YA MILIONI 50 BAADA YA...

GERALD GREEN AKUMBANA NA FAINI YA ZAIDI YA MILIONI 50 BAADA YA KITENDO HIKI

582
0
SHARE

bb
Na Nicasius N Agwanda (Nicasius Coutinho Suso)
Mchezaji mpya wa klabu ya Miami Heat Gerald Green amekumbana na adhabu ya kutozwa faini ya dola za kimarekani elfu ishirini na tano ($25,000) kutokana na kosa la kuonyesha ishara zisizofaa mchezoni ambazo zinachochea hatari na athari kwa jamii nzima.

Tukio zima lilitokea baada ya Green kurusha mtupo wa pointi tatu mara tatu mfululizo katika ushindi wa 110-105 wa Miami heat dhidi ya Washington Wizards siku ya jumatano usiku. Green alionekana akitoa ishara za mtutu wa bunduki na kukatwa shingo kila baada ya mtupo aliorusha.

Katika mchezo huo alifunga pointi 28, na amejiunga na Miami Heat msimu huu akiwa mchezaji huru ambapo alisaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 1.4 ($1.4 million.)

Wapenzi wa kikapu watakuwa wanakumbuka katika vilabu vya Phoenix Suns, Minnesota Timberwolves, Dallas Mavericks, Houston Rockets, Indiana Pacers, New Jersey Nets (sasa Brooklyn Nets) na Boston Celtics akiwa moja ya wachezaji waliochezea vilabu vingi kwa muda mfupi.

Huku pia akiwa kipenzi cha mashabiki wengi wa mchezo huo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kudunk, ambapo alishinda ubingwa wa kudunk wa mashindano yanayoandaliwa na sprite kwa jina la Sprite Slam Sunk, mwaka 2007 katika wiki ya mastaa wa NBA, maarufu kama NBA ALL STAR.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here