Home Kimataifa DANNY GRANGER NJE YA KIKOSI CHA DETROIT PISTONS

DANNY GRANGER NJE YA KIKOSI CHA DETROIT PISTONS

600
0
SHARE
akiwa na Indiana Pacers
akiwa na Indiana Pacers
akiwa na Clippers
akiwa na Clippers
akiwa Miami Heat
akiwa Miami Heat

Na Nicasius N Agwanda ( Nicasius Coutinho Suso)

Kila klabu imeendelea na kujiweka sawa katika kambi zao kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya kikapu nchini Marekani na taarfa zilizotoka jumatatu ya leo ni kuwa klabu ya Detroit Pistons ambayo nayo ilikuwa katika presha ya kukamilisha idadi inayotakiwa ya wachezaji 15 peke yake kwa ajili ya msimu mpya imeamua kuachana na veterani Danny Granger (32) ambaye pia inasemekana kuwa kapata majeraha ya mguu wake hivyo atatakiwa kuwa nje ya mchezo huo kwa takribani mwezi mzima ili atibu majeraha yake.

Majeruhi inasemekana ndio sababu kubwa ya kuachwa kwake na klabu hiyo kwani alishindwa kuwa fiti kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, hivyo kuachwa na kupisha idadi ambayo nayo sasa imekamilika idadi ya wachezaji 15.  Hivyo baada ya kutibu majeraha atarejea kwa ajili ya kutafuta timu ya kujiunga nayo.

Danny Granger atakuwa anakumbukwa na wapenzi wengi wa mpira wa kikapu kutokana na uwezo wake hasa kipindi chake akiwa na klabu ya Indiana Pacers aliyoitumikia sana na kuweka nembo ya jina lake pale, kisha Los Angeles Clippers na Miami Heat.  Kwa zaidi ya miaka 10, amecheza michezo 586 na kuwa na wastani wa point 17 kwa mchezo.

Msimu wake bora kabisa ulikuja akiwa na klabu ya Indiana Pacers msimu wa 2008-2009 ambapo alikuwa na wastani wa pointi 25.8 kwa mchezo, na kupelekea kupigiwa kura zilizotosha yeye kuingia katika timu ya mastaa wa kanda ya mashariki na kushiriki mchezo maarufu wa mastaa unaoitwa NBA ALL STAR GAME.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here