Home Kimataifa AUBAMEYANG ATOA SIRI YAKE YA KUFUNGA HAT-TRICK YA PILI

AUBAMEYANG ATOA SIRI YAKE YA KUFUNGA HAT-TRICK YA PILI

591
0
SHARE

997133_toptease_article_desktop_com

Mmoja kati ya mastaa wakubwa ambao wanaoing’arisha ligi ya Bundesliga ni Aubameyang ambae anatupia magoli ya kutosha nyavuni na kuisaidia club yake ya Borussia Dortmunda. Ukitaka kumcheki huyu jamaa kwenye Bundesliga, Startimes ndio pekee wanaokuonyesha live mechi za ligi hii.

Mchezaji hatari wa Borussia Dortmund Aubameyang alifunga magoli matatu akiwa kwenye mechi dhidi ya FC Augsburg. Kwenye hat trick hiyo Auba alifikisha magoli 20 kwenye msimu huu.

Kumbe alivyokua uwanjani anacheza hiyo mechi alikua na motivation nyuma yake. Akiwa kwenye interview na waandishi wa habari Auba alifichua siri ambayo ilikua ina msukuma uwanjani.

“Jana nili-bet na kaka yangu kwamba nitafunga hat trick nyingine. Sasa ilibidi nifanikishe kufunga magoli yake ili nimshinde kwenye bet yetu. Ninafurahi nimefunga magoli matatu tena na ilikua ni muhimu tumeshinda mechi ile”

Pia alivyoulizwa kuhusu kufunga magoli mengi msimu huu Auba alisema, “Siri yangu ni kufanya mazoezi sana, kupumzika nyumbani hasa kwa kulala. Tunacheza mechi kila baada ya siku tatu ni muhimu sana kupumzika vizuri”

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here