Home Kimataifa MAN UNITED VS MAN CITY NI VITA YA PESA

MAN UNITED VS MAN CITY NI VITA YA PESA

2197
0
SHARE

Mn U vs Man City

Mchezo wa ‘Manchester Derby’ unaozikutanisha Manchester United dhidi ya Mnchester City unatajwa kuwa ni moja kati ya michezo ghali zaidi duniani kutokana na kuwakutanisha wachezaji waliosajiliwa kwa gharama kubwa zaidi.

Mchezo huo ambao utapigwa Jumapili (leo) kwenye dimba la Old Trafford, utawakutanisha wachezaji wa vikosi vya kwanza (starting XI) ambao kwa jumla ya timu zote mbili thamani yao ni £152m.

Man U vs Man City 2

Kikosi cha Manchester United kina jumla ya thamani ya £264.5m wakati kikosi cha Manchester City chenyewe kinathamani ya £281.1m. thamani hiyo  ikiwa ni wachezaji ambao wanaanza kwenye vikosi vya kwanza vya timu hizo.

Kevin De Bruyne Mchezaji wa Manchester City aliyenunuliwa kwa thamani ya  £55m kutoka klabu ya  Wolfsburg
Kevin De Bruyne Mchezaji wa Manchester City aliyenunuliwa kwa thamani ya £55m kutoka klabu ya Wolfsburg

Wakati thamani ya wachezaji wanaotarajiwa kuanza kwenye vikosi vya Man U na Man City ikiwa ni £152m. Kuna wachezaji wengine ambao wako nje ya mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali huku wengine wakianzia kwenye benchi.

Anthony Martial mchezaji wa Manchester United ambaye klabu yake ililazimika kutoa kiasi cha  £58m kumnasa kutoka klabu ya Monaco
Anthony Martial mchezaji wa Manchester United ambaye klabu yake ililazimika kutoa kiasi cha £58m kumnasa kutoka klabu ya Monaco

Sergio Aguero, David Silva, Samir Nasri, Marouane Fellaini, Luke Shaw na Nicolas Otamendi ni wachezaji ambao hawapo kwenye vikosi vya kwanza wanaotengeneza thamani ya £152m.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here