Home Kimataifa WEWE NI SHABIKI WA NBA….JE UNAYAJUA HAYA.

WEWE NI SHABIKI WA NBA….JE UNAYAJUA HAYA.

443
0
SHARE

NNDS

Je wajua kuwa huu ndio utakuwa msimu wa mwisho kwa klabu ya Sacramento Kings kutumia uwanja wake wa Sleep Train Arena, na klabu hiyo yenye wachezaji mashuhuri kama Ruddy Gay na Demarcus Cousins itahamia katika uwanja wa Golden 1 Center. Hivyo mchezo wa mwisho kutokana na Ratiba kuchezwa katika uwanja wa Sleep Train Arena utakuwa dhidi ya Oklahoma City Thunder mnamo April 9.

nn1

Vilabu kadhaa pia msimu huu vimeamua kubadili muonekano wa jezi zao, ikiwemo vilbu vya Milwaukee Bucks, Los Angeles Clippers, Philadelphia 76xers, Atlanta Hawks na Toronto Raptors.

Mchezaji mkubwa kabisa kwa sasa katika NBA ni Andre Miller wa Minnesota Timberwolves mwenye umri wa miaka 39 huku na mchezaji mdogo kabisa katika msimu huu wa NBA ni mchezaji mpya katika NBA Devin Booker wa Phoenx Suns mwenye umri wa miaka 18. Nat Hickey anashikilia rekodi ya kucheza NBA akiwa na umri mkubwa zaidi ambao ulikuwa ni miaka 46 huku mchezaji mdogo zaidi akiwa Andrew Bynum ambaye alicheza NBA akiwa na miaka 18na siku 6.

nn2

Kocha wa San Antonio Spurs, Greg Popovich ndio kocha aliyekaa nba kwa muda mrefu zaidi kwa sasa akiwa na miaka 19 pia ndio kocha aliyeshiriki michezo mingi zaidi akiwa na michezo 1492 kibindoni, akiwa pia ndiye aliyeshinda michezo mingi zaidi 1022 huku pia akiwa ndiye aliyefungwa michezo mingi zaidi 470.

nn3

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here