Home Kitaifa SIMBA SC IMECHEZA VIZURI KATIKA MECHI 1 TU, WAKAPOTEZA, KIWANGO CHA KERR...

SIMBA SC IMECHEZA VIZURI KATIKA MECHI 1 TU, WAKAPOTEZA, KIWANGO CHA KERR KINAKIDHI MATARAJIO

558
0
SHARE

????????????????????????????????????

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam

Dylan Kerr ameisimamia Simba SC katika gemu 7 za ligi kuu Tanzania Bara msimu huu na kufanikiwa kuisaidia kupata ushindi mara tano na kupoteza michezo. Kichapo cha 1-0 kutoka kwa Tanzania Prisons ni cha kwanza katika michezo mitatu walikwisha cheza ugenini msimu huu. Simba ilishinda 1-0 dhidi ya timu iliyopanda daraja African Sports kisha wakaendeleza mwanzo ‘wa kuvunja rekodi’ katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya kuishinda 2-0 JKT Mgambo katika gemu ya pili.

Wakarudi nyumbani-Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuishinda 3-1 timu ya Kagera Sugar. Kufikia gemu hizi tatu kila shabiki wa Simba alikuwa amepagawa na mwanzo wa kuvutia wa timu yao. Kichapo cha 2-0 kutoka kwa Yanga SC katika gemu ya nne hakikuonekana kuwachanganya sana Simba zaidi wakaendelea kusaka ushindi na kuishinda Stand United kwa goli 1-0.

Katika gemu tatu za nyumbani walifanikiwa kushinda mara mbili na kupoteza mechi moja. Tangu awali nimekuwa nikisema kuwa klabu hiyo haichezi vizuri licha ya kushinda mechi zake za mwanzo. Ni jambo la kawaida timu kushindwa kucheza vizuri lakini ikapata matokeo. Bila shaka ndiyo sababu kubwa iliwafanya wapenzi wa Simba kutofuatilia uchezaji wa timu yao hata pale ilipokuwa ikicheza vibaya.

Kufungwa na Tanzania Prisons kulikuja siku tatu baada ya timu hiyo kuishinda Mbeya City FC katika uwanja huo huo wa Sokoine, Mbeya. Simba ilicheza kwa kiwango cha chini katika gemu dhidi ya Sports, Mgambo, Stand na City lakini walifanikiwa kushinda na mechi pekee waliyocheza vizuri ni ile dhidi ya Yanga ambayo walifungwa.

Kerr ameshindwa kuwa na timu ya kudumu. Ameshindwa kutengeneza kikosi cha uhakika cha wachezaji 11. Kiasi amefanikiwa kutengeneza safu ya ulinzi ambayo imekuwa na wachezaji walewale katika gemu nyingi lakini kuanzia safu ya kiungo kuelekea ile ya mashambulizi raia huyo wa Uingereza ameshindwa kuipanga vizuri timu yake.

Katika mechi ya City alimuanzisha Abdi Banda katika wing ya kushoto. Ni kweli Banda anaweza kucheza namba 3, 6, 8 na 11 lakini akiwa ametoka katika majeraha mfululizo Kerr hakutakiwa kumpanga katika nafasi hiyo. Peter Mwalyanzi wengi walimtazama kama mchezesha-timu wa uhakika. Alicheza vizuri dhidi ya Sports na Mgambo lakini amekuwa mchezaji asiye na uhakika wa kuanza mechi hivi sasa.

Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Awadh Juma na Mwalyanzi ilionekana wakicheza kwa viwango vya wastani. Musa Mgosi ameendelea kucheza kwa kiwango dhaifu ni Hamis Kiiza pekee ambaye timu inaweza kusema ni mshambuaji wa kutumainiwa lakini ni vyema pia wachezaji wengine wangekuwa katika kiwango kizuri wakati huu Kiiza akiwa na majeraha.

Simba inashindwa kutengeneza nafasi za kufunga licha ya Kerr kupendelea kuwatumia wachezaji wengi wa nafasi ya kiungo. Kwanini timu inacheza vibaya na kushinda?. Hii ni ligi wakati mwingine timu inahitaji hata goli la mkono ili kupata alama tatu muhimu. Azam FC pia haichezi vizuri lakini msisitizo mkubwa wameuweka katika kuhakikisha wanashinda kila mechi kwa namna yoyote ile.

Kerr anaanza ‘kupigwa na dhoruba’ na kama timu yake itashindwa kuifunga Coastal Union katika gemu ijayo ‘mawimbi’ yakaanza kumsumbua na si ajabu watu wakaanza kuhoji uwezo wake. Ushindi ulimpunguzia kuchunguzwa lakini kama timu itaendelea kuporomoka katika msimamo wengi hawatamtaka.

Simba imecheza vizuri katika gemu 1 tu dhidi ya Yanga msimu huu na wakachapwa lakini wamecheza vibaya na kuzishinda, Sports, Mgambo, Kagera, Stand na Mbeya City, vipi Kerr anaweza kuwafikisha wanapotaka kufika?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here