Home Kimataifa KUELEKEA MSIMU MPYA WA NBA…HAYA NI MAMBO YA MSINGI YA KUJUA

KUELEKEA MSIMU MPYA WA NBA…HAYA NI MAMBO YA MSINGI YA KUJUA

671
0
SHARE

covvv

Kuelekea msimu mpya wa NBA, wachezaji kadhaa hatutowashuhudia tena katika NBA baada ya kustaafu kucheza mchezo huo ambao ni Shawn Marion ambaye alipata umaarufu zaidi baada ya kushinda taji na klabu ya Dallas Mavericks msimu wa mwaka 2011 akiwa kaitumikia NBA kwa misimu 16.

nba1

Mrusi Andrei Kirelenko naye amestaafu kucheza NBA baada ya misimu 13 katika ligi hiyo. Mwingine ni moja ya wachezaji wanaopenda kuchora michoro mingi ya tattoo, Kenyon Martin aliyecheza kwa misimu 15, Stephen Jackson yeye anastaafu akiwa amecheza misimu 14 huku akishinda taji la NBA mwaka 2003 na klabu ya San Antonio Spurs chini ya kocha asiyeeleweka Greg Popovich, Elton Brand yeye amestaafu baada ya misimu 16 na wa mwisho ni Jason Richardson yeye akiwa  na idadi ya misimu 14 mpaka anastaafu.

nba2

Katika kuelekea msimu huu pia vilabu kadhaa vimetimua makocha wao, Oklahoma City Thunder wamemfukuza Scott Brooks baada ya kuwa naye kwa misimu saba na kumuajiri Billy Donovan.

nba3

Baada ya kuwa naye kwa takribani misimu 5, klabu ya New Orleans Pelicans ilimfuta kazi Monty Williams na kumuajiri Alvin Gentry ambaye katoka kushinda ubingwa akiwa kocha msaidizi wa Golden State Warriors.

nba4

Orlando magic imeachana na kocha wake Jmaes Borrego na kumleta Scott Skiles. Nafasi ya Thom Thibodeau katika klabu ya Chicago Bulls imechukuliwa na Fred Hoiberg, Denver Nuggets wamemuajiri Michael Malone mahala pa aliyekuwa kocha wa muda Melvin Hunt, na Minnesota Timberwolves imempumzisha kocha wake Flip Saunders kutokana na maradhi na nafasi yake imeshikwa kwa muda kocha msaidizi Sam Mitchell.

Na Nicasius N Agwanda (Nicasius Coutinho Suso)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here