Home Kitaifa KOCHA WA SIMBA ATOA LA MOYONI KUHUSU MAGULI

KOCHA WA SIMBA ATOA LA MOYONI KUHUSU MAGULI

838
0
SHARE
Elius Maguli (kushoto) akishangilia moja ya goli lake na mchezaji mwenzake wa Stand United Haruna Chanongo
Elius Maguli (kushoto) akishangilia moja ya goli lake na mchezaji mwenzake wa Stand United Haruna Chanongo
Elius Maguli (kushoto) akishangilia moja ya goli lake na mchezaji mwenzake wa Stand United Haruna Chanongo

Mshambuliaji hatari wa Stand United,  Elius Maguli ana mabao manane katika Ligi Kuu Bara na ndiye kinara wa ufungaji, Kocha wa Simba, Dylan Kerr, amesema uwezo wa mchezaji huyo ni aibu kwao. 

Kabla ya kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu, Simba iliamua kuachana na Maguli ambaye amefunga mabao sawa na yale ya timu hiyo, kwa madai kuwa uwezo wake ni mdogo uwanjani. 

Kerr, raia wa Uingereza, amesema kuwa, Maguli anastahili kupongezwa kwa kile anachofanya uwanjani na mafanikio yake ni aibu kwa Simba ambayo ilimuacha. 

Maguri pita telela“Maguli anafanya vizuri kwa kufunga mabao nane hadi sasa, ni aibu kwa Simba,” alisema Kerr na alipoulizwa inakuwaje anasema aibu kwao wakati naye alishiriki kwenye kumuacha, alisema: “Kusema kweli ni yeye mwenyewe ndiye aliyetaka kuondoka Simba.” 

Katika kikosi cha Simba anayeongoza kwa ufungaji ni Hamis Kiiza aliyefunga mabao matano na wengine waliofunga moja-moja ni  Juuko Murshid, Joseph Kimwaga na Justice Majabvi. 

Chanzo: Salehjembe.blogspot.com

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here