Home Kimataifa JAHAZI LA CHELSEA LINAELEKEA PABAYA!!

JAHAZI LA CHELSEA LINAELEKEA PABAYA!!

613
0
SHARE

Chelsea vs West Ham

Mambo bado yameendelea kuwa magumu kwa timu ya Chelsea FC chini ya kocha Jose Mourinho baada ya leo tena kukubali kibano cha goli 2-1 mbele ya West Ham United kwenye mwendelezo wa mechi za ligi ya England maarufu kama EPL.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni miongoni mwa London Derby ukizihusisha timu zote zinazotoka kwenye jiji hilo, mchezo ulipigwa kwenye dimba la Upton Park uwanja wa nyumbani wa West Ham ambao leo walikuwa ni wenyeji wa Chelsea.

Mauro Zarate alianza kuifungia Chelsea goli la kwanza dakika ya 17 kipindi cha kwanza lakini Gary Cahill akaisawazishia Chelsea goli hilo dakika ya 56 kipindi cha pili. Andy Carroll akapeleka msiba darajani baada ya kupachika bao la pili kwa upande wa West Ham dakika ya 79 na kuihakikishia timu yake ushindi wa nyumbani.

Mourinho alikuwa jukwaani akishuhudia timu yake ikipoteza mchezo kutokana na kutumikia adhabu kutoka chama cha soka nchini England kwa kuwatolea lugha za kejeli waamuzi.

Mourinho JukwaaniNemanja Matic alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 45 baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano na kuiacha timu yake ikicheza pungufu kwa dakika zote 45 za kipindi cha pili.

Mbali na Chelsea, West Ham tayari imeshatoa vipondo kwa vigogo vingine vya ligi hiyo kama Arsenal 2-0, Liverpool 3-0 na Manchester City 2-1.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here