Home Kitaifa FRIENDS RANGERS BINGWA MAGUFULI CUP

FRIENDS RANGERS BINGWA MAGUFULI CUP

489
0
SHARE
Wachezaji wa Friends Rangers wakiwa wameinua kombe lao la Magufuli Cup baada ya kuichapa Burudani FC kwa goli 2-1

Bao kutoka kwa mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Emanuel Gabriel ‘Batistuta’, ‘Batigoo’ pamoja na Ally Kaijage yameisaidia timu ya Friends Rangers kuchukua ubingwa wa Magufuli Cup kwa kuichapa Burudni FC kwa bao 2-0 kwenye mchezo wa fainali wa michuano hiyo uliopigwa kwenye uwanja wa Bandari, Tandika.

Mchezo huo uliokuwa wa kuvutia huku mashabiki lukuki wakiwa wamejitokeza kushuhudia pambano hilo, ulianza kwa kasi kwa timu zote kutaka kujihakikishia ushindi wa mapema.

Mchezaji wa Friends Rangers (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa Burudani FC (kulia)
Mchezaji wa Friends Rangers (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa Burudani FC (kulia)

Burudani ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kipindi cha kwanza lililofungwa na Paul Ndauka lakini Emanuel Gabriel akaisawazishia Friends Rangers muda mchache kabla ya mapumziko.

Wakati zikiwa zimesalia dakika chache mchezo kumalizika, Ally Kaijage aliifungia Freiends Rangers bao ambalo liliufanya uwanja mzima kusimama kushangilia goli hilo kutokana na jinsi Kaijage alivyofunga goli hilo kwa ufundi wa hali ya juu.

Mashabiki waliojitokeza kushuhudia fainali ya Magufuli Cup kwenye uwanja wa Bandari, Tandika
Mashabiki waliojitokeza kushuhudia fainali ya Magufuli Cup kwenye uwanja wa Bandari, Tandika

Mshindi wa michuano ya Magufuli Cup amejinyakulia kombe pamoja na shilingi milioni 7,500,000, mshindi wa pili ameondoka na shilingi 5,500,000 huku mshindi wa tatu akiondoka na shilingi 3,550,000 wakati kila timu iliyoshiriki michuano hiyo ikipata shilingi 500,000.

Madee kwa niaba ya kundi la muziki la Tip Top Connections ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo amesema, mashindano hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa huku akizishukuru timu zote zilizoshiriki pamoja na mashabiki na wadau wa soka kwa kudumisha amani kipindi chote cha mashindano hayo.

Msanii wa kundi la Tip Top Connections Madee akizungumza mara baada ya mchezo wa fainali kumalizika kwenye uwanja wa Bandari
Msanii wa kundi la Tip Top Connections Madee akizungumza mara baada ya mchezo wa fainali kumalizika kwenye uwanja wa Bandari

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here