Home Kimataifa TUMUOMBEE LEGENDARI MDACHI JOHAN CRUYFF

TUMUOMBEE LEGENDARI MDACHI JOHAN CRUYFF

467
2
SHARE
Nyota wa zamani wa Barcelona, Johan Cruyff (kulia) akimkabidhi jezi yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) wakati kikosi cha magwiji wa Barcelona kilipomtembelea Rais huyo Ikulu mjini Dar es Salaam mwezi April mwaka huu

Mkongwe wa zamani wa vilabu vya Ajax na Fc Barcelona, mholanzi Johan Cruyff amegundulika na kansa ya mapafu baada ya kufanyiwa vipimo katika hospitali mjini Barcelona hivi karibuni.

Cruyff ambaye alitwaa ubingwa wa Ulaya na klabu ya Ajax mara tatu mfululizo huku akitwaa pia tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or mwaka 1971 amegundulika na kansa hiyo huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Johan Cruyff ambaye alitamba sana katika miaka ya 1970 alikua ni mvutaji mkubwa wa sigara kabla ya kupata tatizo la kiafya na baadala yake akaacha na kuwa balozi wa ant-smoking mwaka 1991.

Taarifa mjini Barcelona zinasema kuwa kutokana na heshima yake na familia, hakutakua na taarifa zozote hivi punde kupisha uchunguzi zaidi wa kiafya kwa fundi huyu wa mpira wa zamani wa Ajax, Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi.

Tayari director wa Ajax Edwin Van Dersar ametuma salamu za pole na kila la kheri kwa legendari huyo huku Barcelona pia wakitoa pole kwa familia na Cryuff mwenyewe kwa tatizo hilo kubwa la kiafya.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here