Home Kimataifa MESSI AELEZEA UADUI WAO NA CRISTIANO RONALDO

MESSI AELEZEA UADUI WAO NA CRISTIANO RONALDO

728
0
SHARE

Messi vs Ronaldo 1

Kabla haujasoma hii story kumbuka kwamba hawa jamaa wanapeana mikono kwenye kila mechi ya El Classico ya La Liga ambapo wanakutana Real Madrid Vs Barcelona. Usikubali kupitwa kwasababu kila kitu kinaonekana Live kwenye Azam TV.

Haya sasa tuendelee na story kamili yenyewe.Mshambuliaji Leonel Messi ameshindwa kukanusha kuihama klabu hiyo siku moja huku pia akisisitiza hana uadui na Cristiano Ronaldo wa Madrid.

Messi ambaye alihusishwa na kuhamia Chelsea msimu uliopita kwa kile kilichotajwa kutokua na maelewano mazuri na kocha Luis Enrique, lakini baadaye alitulia na kufunga magoli 58 huku pia akiisaidia Barcelona kutwaa makombe yote matatu iliyoshirikimsimu uliopita.

Alipoulizwa kuhusu siku moja kucheza ligi nyingine, Messi anasema hataki kufikiria mbali zaidi, kwani kwasasa yuko Barcelona na ndicho anachokiwaza.

Kuhusu kama anashindana na Ronaldo, Messi anasema yeye hana uadui na Cristiano na anaamini Cristiano aliyefunga magoli 61 na sasa ndio kinara wa mabao katika historia ya Madrid hana uadui na hashindani nae.

Messi anasisitiza kuwa hawezi kufanya mashindano na mtu mwingine na badala yake anajituma kusaidia kuzipa ushindi timu anazozichezea.

Akiongea kuhusu majeruhi na lini atarejea, Messi anasema hawezi kukadiria ila kikubwa anamsikiliza daktari wake kuona ni lini atakua tayari kurudi uwanjani baada ya kuumia na kutakiwa kuwa nje ya uwanja kwa majuma 7-8.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here