Home Kitaifa KOCHA MWINGINE VPL AONESHWA MLANGO WA KUTOKEA BAADA YA MATOKEO MABOVU

KOCHA MWINGINE VPL AONESHWA MLANGO WA KUTOKEA BAADA YA MATOKEO MABOVU

567
2
SHARE

Mbwana Makata, kocha mkuu wa timu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera

Kocha wa klabu ya Kagera Sugar Mbwana Makatta ametimuliwa kwenye klabu hiyo kufuatia mfululizo wa matokeo mabovu yanayoikabili timu hiyo kwenye mechi zake za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu.

Makatta ameiongoza Kagera Sugar kwenye michezo nane na kufanikiwa kushinda mchezo mmoja tu dhidi ya Mbeya City siku ya ufunguzi wa pazia la ligi kuu msimu huu mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya. Kagera imetoka sare michezo mitatu na kuambulia vipigo kwenye michezo mingine minne iliyocheza.

Kocha huyo ambaye alitwaa tuzo ya kocha bora wa msimu uliopita baada ya kuongoza Tanzania Prisons katika mechi nane na kuinusuru timu hiyo isishuke daraja, alisaini mkataba na Kgera Sugar wenye kipengele kinachoeleza kuwa, endapo atapata matokeo mabovu mfululizo atasitishiwa mkataba wake na klabu hiyo.

Makatta anakuwa kocha wa tatu kuoneshwa mlango wa kutokea msimu huu baada ya aliyekuwa kocha wa JKT Ruvu Fred Felix Minziro kusitishiwa mkataba wake wakati Coastal Union wao pia wakitangaza kuachana na kocha wao Jackson Mayanja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here