Home Kimataifa IKO WAZI KWA SASA…CRISTIANO RONALDO NI BIG BRAND ZAIDI YA MESSI

IKO WAZI KWA SASA…CRISTIANO RONALDO NI BIG BRAND ZAIDI YA MESSI

566
0
SHARE

messi

Cristiano Ronaldo ni mmoja kati ya chapa 10 zenye thamani kubwa duniani kwenye upande wa michezo, lakini kwenye hiii list Lionel Messi hayupo kabisa.

Kutoka kwa Forbes ambao wametengeneza list hii wamesema kwamba thamani ya brand ya kila mchezaji imetokana na pesa nyingi anazolipwa mchezaji huyo kwenye kila kitu ukulinganisha na wastani wa wachezaji kumi ambao wanalipwa pesa nyingi kwenye mchezo wake. Wastani huo umetokana na pesa walizoingiza mwaka jana.

Kwenye hiyo list Cristiano Ronaldo yupo namba 8 na thamani ya brand yake ni £10.4m, namba moja yupo Tigee Woods ambae thamani ya brand Tiger Woods ni £19.5m akifuatiwa na Phil Mickelson kwa thamani ya £18.2m. Listi inaendelea na anaingia mchezaji tennis maarufu Roger Federer ambae jina lake lina thamani ya £17.5. Kwa upande wa Basketball LeBron James ameingia baada ya Federer kwa kuwa na thamani ya £17.5.

Mcheza cricket kutoka India anaitwa Ms Dhoni yupo namba 5 akiwa na thamani ya £14m na namba 6 imeshikiliwa na watu wawili mwanariadha Usain Bolt na mcheza kikapu Kevin Durant ambao thamani yao ni £12m. Baada ya Ronaldo kwa £10.4m anakuja Rory Mcllroy ambae ana thamani ya £8m. Floyd Money anamaliza kwa kuwa na thamani ya £7.5m.

Thamani ya majina ya wana michezo hawa yanatumika sehemu mbalimbali kwenye chapa tofauti ambazo moja kwa moja zinawanufaisha kiuchumi wachezaji hawa.

Ukiacha na hayo yote soka ndio linaanza…wakali hawa wawili Messi na Ronaldo wanaonyesha uwezo wao kupitia Azam Sport HD ya Azam TV. Hakikisha unajiunga ulimwengu wa La Liga kwa gharama nafuu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here