Home Kitaifa CANNAVARO: ALGERIA WAKAWAIDA TU…

CANNAVARO: ALGERIA WAKAWAIDA TU…

449
0
SHARE

CannavaroNahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema, wao kama wachezaji walijitahidi sana kwenye mchezo wa jana dhidi ya Malawi wakiwa ugenini licha ya kufungwa goli moja wakaiwa ugenini Cannavaro ameongeza kuwa walicheza kwa nidhamu ya juu kuhakikisha hawapotezi nafasi ya kuonga mbele.

Cannavaro amesema mpira unakimbia sana kwenye uwanja wenye nyasi za bandia hivyo iliwalazimu kutumia nguvu ningi sana kumiliki mpira ukilinganisha na kwenye viwanja vingine.

“Tulicheza kwa nidhamu kwasababu tulikuwa tunahitaji kulinda matokeo ambayo tuliyapata nyumbani”, amesema Cannavaro.

“Uwanja ulitu-cost kwasababu kwenye uwanja wa nyasi za bandia mpira unakuwa unakimbia sana, watu wa nje hawawezi kujua hilo, inamaana hata ukitaka kumiliki mpira inabidi utumie nguvu na uupoze sana mpira lakini tumejitahidi”.

Cannavaro amesema watu wachukulie mchezo kati ya Stars dhidi ya Algeria ni wa kawaida lakini akisisitiza Stars lazima itumie faida ya kuanzia nyumbani ili ipate magoli ya yatakayowasaidia kwenye mechi ya marudiano.

“Watanzania inabidi watuombee dua kuelekea mchezo wetu dhidi ya Algeria, tuchukulie ni mchezo wa kawaida na kwasababu tunaanzia nyumbani inabidi tupate magoli mengi ili tuweze kufuzu kwenye hatua ya makundi”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here