Home Kitaifa MFUNGAJI BORA WA ZAMAZI WA LIGI YA ZANZIBAR ASEMA VPL NI NOMA…

MFUNGAJI BORA WA ZAMAZI WA LIGI YA ZANZIBAR ASEMA VPL NI NOMA…

502
0
SHARE
Amour Omar 'Janja' straika wa zamani wa JKU ya Zanzibar anaekipiga JKT Ruvu amekiri ligi ya Tanzania bara ni ngumu kuliko ligi ya Zanzibar
Amour Omar ‘Janja’ straika wa zamani wa JKU ya Zanzibar anaekipiga JKT Ruvu amekiri ligi ya Tanzania bara ni ngumu kuliko ligi ya Zanzibar

Na Abubakar Kisandu, Zanzibar

Amour Omar ‘Janja’ shujaa wa zamani wa timu ya JKU, na pia alikuwa kuwa mfungaji bora wa ligi kuu soka Zanzibar misimu miwili mfululizo msimu wa mwaka 2013-2014 akicheza Miembeni ‘wazee wa kwala’, na msimu 2014-2015 akiwa na JKU.

Janja ambaye kwasasa anacheza JKT Ruvu kwenye ligi kuu soka Tanzania bara na ameshacheza mechi tatu lakini bado hajaonesha makali yake ya kupachika mabao.

Mtandao huu umemtafuta Janja baada ya kudokezwa kuwa yupo visiwani Zanzibar na kutaka kujua kwanini hajafunga hata bao moja mpaka sasahivi.

Janja amekiri kuwa ligi ya Tanzania bara ni ngumu kuliko ligi ya Zanzibar, pia Amour amesema kuwa anasumbuliwa na maradhi mbalimbali na ndio mana hata baadhi ya mechi huwa anakosa kucheza, lakini kasisitiza washabiki wake wategemee mazuri kutoka kwake.

Janja ni mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Mtende Renger, Miembeni na JKU na kwasasa yupo JKT RUVU.

Wapenzi wa Yanga hawawezi kumsahau Janja, ambapo Januari 8 mwaka huu kwenye uwanja wa Amaan alifunga bao pekee dakika ya 72 kwa shuti kali lililomshinda kipa Ally Mustafa kwenye mashindano ya Mapinduzi na kuifanya Yanga itolewe kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here