Home Kimataifa Mourinho anajaribu kujifukuzisha? Baada ya kupoteza imani ya wachezaji wake.

Mourinho anajaribu kujifukuzisha? Baada ya kupoteza imani ya wachezaji wake.

724
0
SHARE

Je Jose Mourinho anajaribu kujifukuzisha kazi? Baada ya mahojiano yake yasiyo ya kawaida yaliyotumia dakika 7 baada ya kipigo kutoka kwa Southampton, ilinifanya nishangae. Mourinho aliiambia Sky Sports hana nia ya kuiuzulu na kama kama klabu inataka aondoke, itabidi wamfukuze. Hili ni jambo la ajabu, kwa sababu hakuwa ameulizwa lolote kuhusu hatma yake ndani ya klabu.

Hii ni baada ya miezi mitano tu tangu atwae ubingwa, kulikuwa na uwezekano mkubwa ripota asingeuliza swali kuhusu kufukuzwa.

  
Makocha kwa kawaida huwa hawanaga tabia ya kuanza kuzungumzia neno la ‘kufukuzwa’, kwa sababu mara tu linapoanza kuwa kwenye mazungumzo huwa inakuwa ngumu kuanzisha tetesi. Hivyo ilishangaza kuona Mourinho akianzisha mjadala wa kufukuzwa, na hata akajaribu kutoa ishara ya namna ambavyo alikuwa amejiandaa kuondoka klabuni.

Mara ya mwisho Chelsea ilipomtimua Mourinho ilibidi wamlipe kiasi cha £18m katika fidia. Hivi sasa ndio kwanza yupo ndani ya miezi miwili ya mkataba mpya wa miaka 4. Na ikiwa Chelsea watamfukuza safari hii inaripotiwa itabidi wamlipe kiasi cha £37m kama fidia – japokuwa watu wakubwa kwenye soka wa aina yake wengi huwa hawaendeshwi kimaamuzi na fedha – lakini inawezekana pia namna nzuri ya kuondoka huku unacheka ukielekea benki.

  Baada ya kuzungumzia kuondoka, Mourinho baada ya hapo akazungumzia kwamba yeye ndio manager bora ambaye Chelsea wanaweza kuwa nae. Hivyo akaaichia klabu wakati muhimu kimaamuzi – Ikiwa watamfukuza hivi sasa watakuwa wanajiijingiza kwenye mipangilio iliyofeli. Wangetoa picha kwamba ndani ya klabu ya Chelsea siku zote timu ikifanya vibaya basi huwa ni makosa ya kocha na sio wachezaji, hata kama kwa sasa ni wazi kabisa ni kushindwa kwa wachezaji dimbani ndio kumepelekea hali iliyopo Chelsea kwa sasa.

Kauli za Mourinho hadharani zingesaidia, lakini kwa sasa hayupo katika nafasi ya kuwabana waajiri wake hadharani.

Pili kwa kusema hadharani kwamba wachezaji wajirekebishe, alitoa ishara kwamba klabu inaendeshwa kama nyumba ya vichaa, sehemu ambayo kocha anayejiita bora duniani anaweza asidumu kwa muda mrefu. Labda kitendo chake cha kuongea hadharani kinaweza kudhiti uharibifu wa sifa yake ikiwa kufukuzwa anapokuongelea kutatokea.

  Mourinho hajui wapi kwa kunyamaza wapi kwa kuongea na kitu sahihi cha kuongea, inawezekana hata baadhi ya wachezaji wake wameanza kuchoshwa na tabia zake – wiki iliyopita kuna gazeti nchini Uingereza liripoti kwamba baadhi ya wachezaji wakubwa kikosini walikuwa wamechoshwa na tabia ya Mourinho kuwafanya mbuzi wa kafara wachezaji baada ya matokeo mabaya.

Mourinho atakuwa amesoma taarifa ziliripotiwa kuhusu wachezaji wake. Alipokuwa Real Madrid, Mourinho aliwatuhumu wachezaji wake kwa kuvujisha habari kwa waandishi. Jambo kama hilo sasa limejitokeza Chelsea.

Siku moja baada ya taarifa ya kuwafanya wachezaji ‘mbuzi wa kafara’, Mourinho aliwaambia waandishi wa habari: “Nina uhakika mna watu wambea wanaowaambia nini kinaendelea.”

Kauli hizi zitakuwa sio ngeni kwa mwandishi wa EL Pais – Diego Torres, ambaye alisikiliza kwa umakini kauli zote za kutuhumu wachezaji waliokuwa wanavujisha taarifa katika utawala wa Mourinho ndani ya Bernabeu na akazikusanya na kuziandikia kitabu cha – Mourinho’s time at Madrid, The Special One.

Mourinho alikielezea kitabu hicho kama stori za kusadikika lakini stori hizi za kusadikika zinatoa picha halisi ya matatizo yanayoikumba Chelsea hivi sasa.

Kwa mfano, Torres anadai Mourinho aliwaambia wachezaji wake: “Inabidi ujifunze namna ya kuzuia mashambulizi kwa kila namna, ikiwa utaona ukiruka juu, hutoweza kurudi chini kwenye nafasi yako kwa haraka, basi usiruke. Ikiwa unaona unaweza kwenda sehemu nyingine ya uwanja bila kuweza kurudi kwenye nafasi yako kwa wakati basi usiende bila kujali matokeo ya kitendo hicho.”

Katika timu za Mourinho, kila mchezaji anajua ikiwa timu itaruhusu goli basi hilo goli litakuwa lawama ya wachezaji ambao hawakuwa kwenye nafasi zao wakati goli linafungwa.

Wakati Southampton walipofunga goli lao 3, unaanza kujiuliza yupo wapi Matic? Mtu ambaye kwa kawaida huwa ndio anazima mashambulizi ya namna hilo. Lakini Matic alikuwa kaenda mbele kupiga krosi ambayo haikufanikiwa na kurudi golini mwao – japo alijaribu kukaba akiwa juu lakini hakufanikiwa.

  Matic alitolewa haraka baada ya goli hilo, dakika 28 baada ya kuingia baada ya mapumziko. Mabadiliko hayo yalionekana kama adhabu kuliko suluhisho.

Baada ya hapo Mourinho alizidi kuchanganyikiwa, na kama kawaida yake pale anapokuwa yupo nyuma hasa katika kipindi cha pili – jibu lake huwa ni moja: Kuongeza straika mwingine. Kama akiwa hana straika kwenye benchi, basi humuhamishia beki au kiungo mbele na kucheza mipira mirefu.

Timu yenye kujaa wachezaji wenye uoga wa kushambulia kwa kuogopa kurudi kwenye nafasi zao huwa ni timu yenye kucheza kwa kuzuia, lakini timu ya namna hiyo huwa haifungi magoli mengi. Ni timu ambayo mwishowe hupoteza imani na uwezo wa kufunga. Timu ambayo huamini ukiwa upo nyuma baada ya kipindi cha kwanza, basi mechi ushaipoteza.

Mourinho ana tabia hizo hapo juu. Swali la kujiuliza Je alifikiria namna au mbinu za kuiwezesha timu kupigana na kupata matokeo katika dakika 20 za mwisho, au tayari alishaanza kutengeneza speech yake ya baada ya mchezo iliyodumu dakika 7?

  Mourinho hakumuacha Matic pia ulipofika muda wa kuongelea mabadiliko aliyoyafanya.

“Matic hachezi vizuri, hana kasi anapocheza kwenye ulinzi. Anafanya makosa akiwa na mpira. Hana maamuzi sahihi.” Mourinho alisema alimtoa Matic na sio Oscar au Fabregas kwa sababu Oscar ni mbunifu zaidi na Fabregas anacheza vizuri wakati inapocheza kwa presha.

Hivyo kwa maneno yake ni kwamba sio tu kwamba Matic hayupo kwenye form, bali pia sio mbunifu na kisaikolojia ni mdhaifu. Haya ni maneno ambayo tumeyazoea kuyasikia kwa wachambuzi wenye maneno makali lakini sasa unayasikia kutoka kwa kocha wako.

Baadhi ya wachezaji wangeona huo udhalilishaji na kocha kukosa uaminifu kwa mchezaji wake. Ni vigumu kuweka sawa uhusiano wa kocha na mchezaji baada ya hili na inawezekana Mourinho tayari amepoteza mamlaka/uwezo wa kurudisha hali sawa ndani ya klabu yake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here