Home Kitaifa STARTIMES YAJIVUNIA MABORESHO YA HUDUMA ZAKE KWA WATEJA

STARTIMES YAJIVUNIA MABORESHO YA HUDUMA ZAKE KWA WATEJA

1635
0
SHARE

Startimes

Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayosherehekewa na taasisi pamoja na makampuni mengineyo duniani kote, kampuni inayotoa huduma za matangazo ya luninga kwa dijitali nchini ya StarTimes imesema kuwa imepiga hatua kubwa katika maboresho ya huduma zake.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa wiki hii hutoa fursa ya kipekee ya kupima huduma wanazozitoa kwa wateja na namna ya kuzifanyia maboresho.

“Tunapokutana na wateja wetu ana kwa ana ndivyo hutuwia urahisi kwetu kuweza kujua wanahitaji nini hasa. Ukizingatia ndani ya wiki hii yote wateja wetu wamehudumiwa na wakuu wa vitengo mbalimbali. Kwa mfano kwa sasa tunafanya jitihada nyingi za kusambaza huduma zetu mikoani ili kuwafikia wateja wengi zaidi wa vijijini.” Alisema Bi. Hanif

Amesema kuwa mpaka hivi sasa Kampuni yake imekwishaifikia mikoa takribani 18 nchini Tanzania na mipango ni kusambaza zaidi kila pembe ya nchi.

“Tunatoa huduma zetu kwa bei nafuu zaidi ili kila mtanzania aweze kumudu lengo ikiwa ni kila mmojawapo afurahie ulimwengu wa dijitali nchini.” Alimalizia

Kwa upande wake Meneja wa Operesheni wa StarTimes Tanzania, Bw. Gaspa Ngowi naye amesema kuwa katika kuboresha huduma zao kampuni imeboresha chaneli za michezo kwa kutambulisha vifurushi vipya mahususi kwa wapenzi wa michezo nchini.

Meneja huyo ametaja kuwa vifurushi hivyo ni vya Sports Play na Sports Plus ambavyo amefafanua kuwa ni kama nyongeza ya vifurushi viwili vilivyopo vya Mambo na Uhuru.

“Hivi sasa wateja wetu wa kifurushi cha Mambo wanaweza kujiongeza kwa kuongeza malipo kidogo ya Sports Play ambapo wataweza kujivinjari na ligi za Bundesliga  ya Ujerumani, Serie A ya Italia na Ligue 1 ya Ufaransa ‘Live’ kupitia chaneli za Sports Arena, Fox Sports na Sports Life.”

Vilevile kwa wateja wa kifurushi cha Uhuru nao wanaweza kuongezea malipo kidogo kwa ajili ya Sports Plus ligi hizo hizo kupitia chaneli za Sports Life, Sports Premium na World Football channels.

Bw. Ngowi aliendelea kwa kusema kuwa machaguo ya vifurushi hivi vipya kunaonyesha kujidhatiti kwa kampuni ya StarTimes katika maboresho, ubunifu na kuwajali zaidi wateja wake hususani wapenzi wa soka kuweza kutazama michuano na ligi mbalimbali kwa bei nafuu.

“Siku zote tutabaki kuwa waaminifu kwa wateja wetu kwa kuwapatia huduma za kipekee kutoka StarTimes kwa kuwawezesha kufurahia michezo mbalimbali na tena kwa machaguo ya bei zinazolingana na vipato vyao.” Aliongezea

Bei za kifurushi cha Sports Play ni shilingi 5000/- na Sports Plus ni shilingi 14,000/- tu.

“Hii inamaanisha kwamba kwa wateja wa Mambo ambao wanalipa shilingi 12,000/- itabidi waongezee shilingi 5000- ili kupata kifurushi cha Sports Play na wateja wa Uhuru wanaolipia shilingi 24,000/- itabidi waobgezee shilingi 14,000/- ya kifurushi cha Sports Plus,” alisema Bw. Ngowi na Kumalizia, “Kwa kufanya hivyo wataweza kutazama mechi zote Live na pia kwa wateja wa kifurushi cha Kili kuna ongezeko kidogo la bei kwani wao watalipia shilingi 48,000/- na kuweza kupata chaneli zote za vifurushi vya michezo.”

Akitoa maoni juu ya huduma za StarTimes nchini, mtangazaji na mchambuzi nguli wa masuala ya michezo, Bw. Shaffih Dauda amepongeza sana jitihada za kampuni hiyo katika kuunga mkono shughuli za michezo hususani soka.

Amesema kuwa kuonyesha uthubutu wao katika kudhamini ligi ya daraja la kwanza ni tukio linalohitaji pongezo kubwa sana.

“Kwa muda mrefu kilio cha wapenzi na wadau wa soka nchini ni kupata udhamini kwa ligi ya daraja la kwanza ambayo huibui vipaji vingi zaidi tunavyoviona ligi kuu. Kwa udhamini huu wa StarTimes tunaamini kuwa utaongeza hamasa zaidi, utainua ari na pia kufanya ligii hii kuwa yenye ushindani zaidi ambapo soka la Tanzania litajionea timu nzuri zaidi zikitengenezwa na wachezaji wazuri zaidi wakipatikana ambao si hazina tu kwa ligi kuu bali pia hata kwa timu ya taifa na kimataifa.” Alihitimisha Bw. Dauda

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here