Home Kimataifa Ikiwa atakutwa na hatia, hii ndio adhabu ya kifungo kwa Messi

Ikiwa atakutwa na hatia, hii ndio adhabu ya kifungo kwa Messi

598
0
SHARE

Masaa 24 tangu ilipotoka taarifa kwamba mwanasoka wa FC Barcelona na Argentina Lionel Messi sasa atafunguliwa rasmi mashtaka mahakamani kwa kesi ya kukwepa kodi nchini Hispania – sasa tuangalie ikiwa atakutwa na hatia adhabu atakayopata.
Ikiwa mwanasoka huyo atakutwa na hatia, adhabu ya kifungo cha miezi 22 itamkuta. Mwendesha mashtaka wiki iliyopita alisema Messi hana kesi juu ya ukwepaji kodi kutokana kwamba hakuwa na ufahamu wowote wa vitendo vya baba yake vya kukwepa kodi ya kinachofikia £3.5m kati ya mwaka 2007 na 2009.
Lakini jana Jaji wa mahakama alikubali ushauri wa mwanasheria wa serikali, ambaye alisema Messi inabidi asimame kizimbani kwa makosa matatu ya ukwepaji kodi.

Adhabu ya juu kabisa ya kesi hii ni kifungo cha miezi 22.5 jela.

Hakuna shabiki yoyote wa soka ambae ana tamani mchezaji huyu aende jela. Tunachotaka sisi ni kumuona kwenye La Liga ya Azam TV. Ungana na wajanja wanocheki soka la ukweli kwa beii nzuri.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here