Home Dauda TV VIDEO: KOCHA MSAIDIZI WA MALAWI ASEMA BADO HAWAJAKATA TAMAA…AWEKA WAZI KINACHOMPA MATUMAINI

VIDEO: KOCHA MSAIDIZI WA MALAWI ASEMA BADO HAWAJAKATA TAMAA…AWEKA WAZI KINACHOMPA MATUMAINI

415
0
SHARE
Ramadhani Nsanzurwimo, kocha msaidizi wa kikosi cha Malawi
Ramadhani Nsanzurwimo, kocha msaidizi wa kikosi cha Malawi

Kocha msaidi wa timu ya taifa ya Malawi Ramadhani Nsanzurwimo amesema, bado timu yake haijatoka kwenye mashindano licha kupoteza kwa goli 2-0 ugenini dhidi ya Stars kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa, Tanzania kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Nsanzurwimo ameongeza kuwa tayari wameisoma Stars na kubaini mapungufu kadhaa ambayo watayatumia kwenye mchezo wa marudiano nchini Malawi ili kupata ushindi kwenye mchezo huo.

Kocha huyo amesema kuna wachezaji kadhaa ambao waliwaacha Malawi kwasababu mbalimbali ambao anauhakika wataisaidia Malawi kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo utakaochezwa Octoba 11 mwaka huu.

Angalia video hapa chini ya Nsanzurwimo akieleza matumaini yake taya Malawi kufanya vyema kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Stars.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here