Home Kitaifa TFF YAMPA MKWASA ULAJI

TFF YAMPA MKWASA ULAJI

283
0
SHARE
Kocha mkuu wa Tanzania  'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa amepewa mkataba mpya wa kudumumu kuifundisha timu hiyo wa  mwaka mmoja na nusu
Kocha mkuu wa Tanzania ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa amepewa mkataba mpya wa kudumumu kuifundisha timu hiyo wa mwaka mmoja na nusu

Charles Boniface Mkwasa amepewa mkataba wa kudumu kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia Oktoba mosi mwaka huu na kumalizika  Machi 31, 2017.

TFF imefikia makubaliano hayo na kocha Mkwasa baada ya kuridhika na utendaji wake katika kukinoa kikosi cha timu ya Taifa, ambapo mpaka sasa ameweza kuingoza Stars katika sare ya michezo miwili dhidi ya Uganda na Nigeria.

Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka.

 Naye kocha Mkwassa ameeleza kufurahishwa na makubaliano haya na ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha kiwango cha Timu ya Taifa kinapanda. 

Aidha Kocha Mkwassa ametoa wito kwa wadau wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here