Home Kitaifa MWAMBUSI AJA NA YAKE JUU YA HUKUMU YA NYOSSO

MWAMBUSI AJA NA YAKE JUU YA HUKUMU YA NYOSSO

571
0
SHARE
Juma Mwambusi, kocha mkuu wa Mbeya City ya jijini Mbeya
Juma Mwambusi, kocha mkuu wa Mbeya City ya jijini Mbeya

Kocha mkuu wa Mbeya City Juma Mwambusi amesema ameangalia vizuri video inayoonesha tukio zima la beki wake Juma Nyosso kumfanyia kitendo ambacho si cha kiungwana nahodha wa Azam FC John Bocco na kudai kuwa inabidi TFF ipitie upya video hiyo na kuangalia jinsi Bocco alivyokuwa akimsumbua Nyosso.

Lakini pia ameongeza kuwa, anaiomba klabu yake ya Mbeya City kufatilia sakata hilo ili kuhakikisha haki inatendeka huku akisema kumfungia miaka miwili mchezaji anaetegemea soka kuendesha maisha ni adhabu kubwa sana.

“Nimeangalia ule mkanda na nimejiridhisha kulikuwa na kuchokozwa muda mrefu lakini mchezaji aliweza kuvumilia na kumwambia refaree huyu Bocco ananifanyia vitendo ambavyo si vya kiungwana lakini ukiifatilia DVD yote unaweza kugundua matukio manne Bocco anamchokoza Nyosso ili a-react na kutoka kwenye mchezo”, Mwambusi amesema.

“Lakini tuliweza kumtuliza mchezaji asiwe na tension lakiki ikafika wakati Bocco anamchokoza mbele ya mwamuzi lakini hakuona lile tendo, sasa imepelekea mpaka hukumu yenyewe. Mimi kama mwalimu nimesikitishwa sana na viongozi wangu kwa kutoa hukumu ya jazba bila kufanya uchunguzi yakinifu kujua nini hasa kilikuwa kinapelekea matatizo yatokee”.

“Mimi nimewaambia viongozi wangu kuwa hili suala inabidi tulifatilie na ukiangalia picha za mnato ni tofauti sana na picha ile ya video ambayo inakupa picha halisi”.

“Ukiangalia mechi yenyewe ilikuwa inamambo mengi sana ya kufatiliwa, tumeona Uingereza mchezaji wa Arsenal alitolewa kwasababu ya kufanyiwa vitendo ambavyo si vya kimichezo na mchezaji Diego Costa lakini klabu ilivyolalamika wakapitia upya video wakakuta Diego Costa amesababisha yule mchezaji atolewe kwa kadi nyekundu”.

“Kwahiyo akapata adhabu yule mchezaji aliyesababisha mwenzake apate kadi nyekundu na yule aliyepata adhabu ya kadi nyekundu akaachwa kwasababu siyo kosa lake kosa lilisababishwa na mchezaji mwingine kwa makusudi”.

“Kabla ya ile mechi jina la mwamuzi lilikuwa ni Jocob Adongo, lakini tunaenda uwanjani tunakuta jina la Martin Saanya. Sasa angalia mazingira ya mechi yenyewe, yanatupa shaka sana tulipata goli zuri tu ambalo hata wewe ukirejea video utasikitika sana lakini tumekataliwa”.

“Mambo mengi yametokea kwenye ule mchezo hata Nyosso mwenyewe alikwatuliwa kwa nyuma na sheria za soka zinasema tackling from behind ni red card lakini Bocco kamkanyaga Nyosso hakupata hata kadi ya njano, onyo wa karipio lolote”.

“TFF mimi wametoa maamuzi ya jazba, hukumu ya miaka miwili kwa mcheza mpira mchezaji ambaye anategemea mpira umpe chakula na watoto wake.  Mimi naiambia klabu ifatilie na kupeleka malalamiko yetu TFF au bodi ya ligi waiangalie upya adhabu hii ili tupate haki”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here