Home Kimataifa NEYMAR NI BORA ZAIDI YA RONALDO NA MESSI…NANI KASEMA HIVI?

NEYMAR NI BORA ZAIDI YA RONALDO NA MESSI…NANI KASEMA HIVI?

3775
0
SHARE

neya

Kila siku story inayoleta mdahalo ni kujaribu kujua nani mchezaji mkali kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. Jibu bado halijapatikana ukizingatia Messi kamaliza vizuri msimu uliopita na Cristiano Ronaldo anaelekea kufanya hivyo hivyo msimu huu kwa kasi aliyoanza nayo.

Sasa Roberto Carlos mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil alivyoulizwa swali maarufu sana kuhusu nani mkali kati ya Ronaldo na Messi alisema hivi,“Watu kila siku wanamzungumzia wale wale Messi na Ronaldo lakini ningependa kumzungumzia Neymar. Kwa upande wangu Neymar ni mkali zaidi yao”

“Hao wengine ni wakali pia lakini mimi namchagua Neymar, ukimuangalia Cristiano Ronaldo ni mchezaji ambae anajitengeneza mwenyewe, ana nidhamu ya kazi na anachokifanya kinavutia hivyo hivyo kwa Messi kazi anayofanya ni kubwa hadi anashinda Ballon d’Or.”

Je, ni kweli Neymar ni mkali zaidi ya Messi na Ronaldo?? Jibu lipo kwenye Azam TV ambapo mechi zao zote za La Liga zinaoenekana Live kabisa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here