Home Kitaifa MBEYA DERBY: MWAMBUSI AMESEMA HIVI KUELEKEA ‘MSHIKEMSHIKE’ HUO

MBEYA DERBY: MWAMBUSI AMESEMA HIVI KUELEKEA ‘MSHIKEMSHIKE’ HUO

539
0
SHARE
Juma Mwambusi, kocha mkuu wa Mbeya City ya jijini Mbeya
Juma Mwambusi, kocha mkuu wa Mbeya City ya jijini Mbeya

Kuelekea Mbeya Derby ambayo inazikutanisha timu za mkoa huo ambazo ni Mbeya City FC dhidi ya Tanzania Prisons kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi amezungumzia maandalizi na mipango ya timu yake kuelekea mechi hiyo

Shaffihdauda.com: Unaelekea kwenye mchezo wa Mbeya Derby mchezo ambao huwa ni mgumu na una presha kubwa, umejipanga vipi wewe na timu yako ili kuhakikisha unaibuka na ushindi kwenye mechi hiyo?

Mwambusi: Kama unavyojua ligi imeanza mechi ya kwanza tumepoteza lakini vilevile timu yangu inamchanganyiko wa wachezaji wapya na wale wa zamani wachache. Kwahiyo nachotaka kama mwalimu, ni kuhakikisha narudisha uwiano na uwelewano wa wachezaji uwanjani.

Tumeingia kambini tumechelewa na hatujapata mechi nyingi za kirafiki na mimi kuweza kujua kikosi changu cha kwanza ni kipi, lakini kubwa ni kwamba tumesajili wachezaji vizuri vilevile tumepandisha wachezaji kutoka kikosi cha pili na tunawatumia kwasababu wanajua mfumo wa Mbeya City na baada muda tutakuwa tumetengeneza timu ambayo inaushindani mkubwa.

Tumeanza vibaya kwa kupoteza lakini mchezo wetu wa pili tukashinda goli tatu, lakini mimi nasema bado kunamakosa ambayo vijana wangu wanatakiwa wayapunguze ndani ya uwanja na nawapongeza kwasababu tumeweza kupata pointi tatu na magoli mengi kwenye uwanja wetu wa nyumbani.

Shaffihdauda.com: Ni maeneo gani ambayo umegundua bado yanamatatizo?

Mwambusi: Kwasababu wachezaji bado wapo, kikubwa tunapokwenda nataka wacheze kama timu sitaki kuona mchezaji anacheza kwa kutumia kipaji chake isipokuwa pale ambapo inatokea analazimika kufanya hivyo, lakini nachotaka mimi tucheze kama timu tukimkosa mchezaji mmoja basi akija mchezaji mwingine kusionekane kama kunachezaji flani katoka.

Kama nilivyotengeneza kikosi miaka mitatu iliyopita, ndio nataraji kufanya hivyo. Na hii itawezekana kwasababu wachezaji wanashika mafunzo, wanaelewa uwanjani lakini hata ‘Yeusalemu’ haijajengwa siku moja, tunataka tufanye subira ili tuweze kufika kule tunako tegemea.

Shaffihdauda.com: Umesema mlichelewa kuingia kambini, mliingia kambini ukiwa umebaki muda gani kabla ya kuanza kwa ligi?

Mwambusi: Mimi maranyingi huwa napenda kupata wiki sita, lakini sasa sikupata wiki sita nilipata wiki nne. Wiki nne maana yake nzuri kwa ajili ya maandalizi tu lakini si kwa practical, mambo ya factinal za wachezaji uwanjani, friend matches ili kuweza kurekebisha makosa kabla ya kuanza kwa ligi

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here