Home Kimataifa KUELEKEA UEFA…AGUERO NJE YA KIKOSI CHA MAN CITY

KUELEKEA UEFA…AGUERO NJE YA KIKOSI CHA MAN CITY

1547
0
SHARE
Kun Aguero 1
Vinara wa EPL Manchester City ya, leo wanatarajia kushuka dimbani kucheza mechi yake ya kwanza ya hatua ya makundi ya klabu Bingwa barani Ulaya, dhidi ya ‘Kibibi kizee cha Turin’, Juventus ya Italia, huo ukiwa ni mchezo wa kwanza wa kundi D kwa klabu zote mbili.
Sergio Aguero ‘Kun’
 
Manchester City, tayari wamethibitisha kumkosa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayekipiga klabuni hapo, Sergio Aguero ‘Kun’ baada ya kusumbuliwa na jeraha la goti. 
Aguero ataukosa mchezo huo, baada ya kupata jeraha la goti katika mechi dhidi ya Crystal Palace, mechi iliyomalizika kwa Man City kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
David Silva
 
Mshambuliaji huyo alipata jeraha la goti baada ya kufanyiwa faulo mbaya na Scott Dann, hivyo hatakuwepo katika mechi hiyo, pamoja na hali hiyo, kocha wa klabu hiyo Manuel Pellegrini, amethibitisha kurejea kwa David Silva na Raheem Sterling licha ya kukosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Crystal Palace.
Raheem Sterling

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here