Home Kitaifa Adolf Rishard; Wachezaji Stars Wafanane na Walimu wao….

Adolf Rishard; Wachezaji Stars Wafanane na Walimu wao….

608
0
SHARE

tino 2

Alicheza mipambano miwili kati ya mitatu ya Taifa Stars na Nigeria wakati timu hizo mbili zilipokutana mara tatu mwaka 1980. Machi 8, Stars ilipigwa 3-1 katika mchezo wa hatua ya makundi wa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1980, michuano ambayo ilifanyika Nigeria ndiyo pekee kwa Stars kuwahi kucheza hadi sasa.

Namzungumzia mlinzi mahiri wa zamani wa timu ya Taifa Stars, Adolf Rishard ambaye kwa sasa ni mwalimu mzoefu wa kandanda nchini. Desemba 6, 1980 Stars ililazimishwa sare ya kufungana 1-1 jijini Lagos katika mchezo wa kwanza hatua ya mtoano kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia. Adolf alishiriki katika michezo yote hiyo kabla ya kukosekana katika mchezo wa marejeano Disemba 20, 1980 kutokana na kuwa na majeraha.

Kuekelea mchezo wa Jumamosi hii kati ya Stars na Nigeria kuwania nafasi ya kufuzu kwa CAN 2017 nimefanya mahojiano na mwalimu Adolf ambaye amezungumza kwa kirefu mambo muhimu ya kuzingatiwa ili kuhakikisha Stars inashinda gemu hiyo…..

www.shaffihdauda.co.tz; Mwalimu unazungumziaje gemu ya kesho dhidi ya Nigeria?

Adolf; Nimeitazama Nigeria katika michezo yao ya hivi karibuni, nilitazama gemu yao na Chad. Mimi naona tunaweza kabisa. Tanzania tuna bahati kuwa na wachezaji wenye vipaji, uwezo na jopo la makocha ambao wapo a timu hivi sasa, yaani, Hemed Morocco, Charles Boniface na Abdallah Kibadeni ni watu ambao kusema kweli nawaamini kabisa wanaweza kuifuatilia gemu vizuri.

tino

Sioni kama kuna ugumu sana wa kushinda mechi, ni wachezaji wawe watulivu na wajiamini waweze kutekeleza yal ambayo watakuwa wamefundishwa. Najua walimu watakuwa na mikakati ya kuhakikisha tunashinda, jambo kuu ni wachezaji ambao ni watendaji wa yale ambayo wamefundishwa na makocha. Wachezaji wajiamini, wawe mahiri na ueledi katika kutekeleza majukumu yao. Aamini kabisa tunao vijana ambao wanaweza kupambana kulingana na timu hii ya Nigeria ambayo nimeiona.

www.shaffihdauda.co.tz; Tumekuwa na kawaida ya kufungwa magoli katika dakika za mapema, unaweza kukuta ndani ya dakika Saba za mwanzo tayari tumefungwa au dakika Tano mara baada ya kuanza kipindi cha pili tuna ruhusu goli kwanini huwa hivi?

Adolf; Unapocheza mechi gumu kama hii na ukaanza kufungwa mapema tena tukiwa nyumbani, kwa tabia za wapenzi wetu wa mpira kusema kweli hukatisha sana tama. Hilo unalosema ni kweli kabisa. Tumewahi kucheza na Nigeria U20, NDANI YA DAKIKA Saba hizo unazosma tulikuwa tayari tumefungwa goli 1-0.

Goli ambalo tuliwapa kabisa kwa sababu mlinzi wetu ndiye aliyetoa pasi ya goli kwa straika wa timu ya Nigeria kwa hiyo goli lile peke yake tena ndani ya dakika kumi za mwanzo lilitufanya tucheze kama ‘ watumwa’. Kwa sababu sisi tunacheza nyumbani na tabia za wachezaji wetu, tabia za mashabiki wetu, wachezaji wajitahidi kwa kweli ndani ya dakika ambazo unazisema tuwe tumepata goli sisi.

www.shaffihdauda.co.tz; Umecheza mara mbili dhidi ya Nigeria kama mchezaji, pia umewahi kuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Vijana wakati ilipocheza na Nigeria miaka mitatu iliyopita, Je, ubora wa Nigeria uko katika maeneo gani?

Adolf; Wako na ari, pia wako vizuri katika ‘ fitness’, kiufundi. Wana kawaida ya ‘ kuiburuza gemu’ –kulazimisha lazima iwe yao. Ana wachezaji ambao wamezoea kucheza mechi za Kimataifa kila siku. Unajua ukiwa a wachezaji wanaocheza mpira nje ya nchi yako ( wachezaji wa kulipwa), wale kila siku wanacheza mechi nyingi ngumu kuliko.

Sasa sisi kwetu tuna wachezaji ambao wanacheza ligi yetu ya ‘ kirafiki’, ligi ambayo kusema kweli siyo ngumu hivyo kulinganisha na ligi nyingine kwa hiyo wachezaji wao wana uzoefu kuliko sisi lakini, hiyo si kigezo.

Sisi pia tuna uwezo, wachezaji wetu wana uwezo nah ii timu iliyopo sasa hivi ina wachezaji ambao huu ni wakati wao wa kucheza. Naamini kabisa wachezaji wetu wakiwa na ari, kuwa watulivu a wakiamua tunaweza kushinda. Wachezaji kama wataenda uwanjani kwa kujua wako nyumbani nadhani tuna weza kufanya vizuri.

www.shaffihdauda.co.tz; Hii ni mechi ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi Stars kusimamiwa na mwalimu Mzawa, una ushauri gani kwa benchi letu la ufundi?

Adolf; Kusema kweli mimi naamini kabisa kuwa Mkwassa anawza na watu ambao wako neye wanaweza. Morocco, Kibadeni ni watu ambao kwanza wanafahamu mpira, wana kiwango kizuri cha kufundisha mpira, cha msingi tu ni kuhakikisha kwamba wachezaji wanafanana na mwalimu.

Mimi aamini walimu lakini kusema kweli wasiwasi wangu mkubwa ni wachezaji, je, watafanana na falsafa, maelekezo na mtazamo wa mchezo kwa kufuata maagizon ya walimu, lakini kama wachezaji watafanana na mawazo ya makocha huku wakicheza na fikra zinazotoka katika benchi la ufundi tunaweza kushinda.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here