Home Kitaifa MBWEMBWE: “FARU LAZIMA ICHUKUE NDONDO CUP 2015”

MBWEMBWE: “FARU LAZIMA ICHUKUE NDONDO CUP 2015”

302
0
SHARE
Kocha mkuu wa Faru Jeuri Supia Mbwembwe akihojiwa na Azam TV mara baada ya mchezo kati ya timu yake ya Faru Jeuri hidi ya Makumba FC
Kocha mkuu wa Faru Jeuri Supiya Mbwembwe akihojiwa na Azam TV mara baada ya mchezo kati ya timu yake ya Faru Jeuri hidi ya Makumba FC

Kocha wa Faru Jeuri Supiya Mbwembwe ambaye pia golikipa wa zamani wa Simba SC amesema ubingwa wa Ndondo Cup msimu huu lazima auchukue kutokana na kikosi alichonacho, mazoezi wanayofanya, mipango iliyopo na historia ya timu hiyo kwenye michuano mbalimbali.

“Kombe hili lazima nilichukue kwasababu hii ni fainali yetu ya 10 kucheza na kati ya fainali hizo tumechukua vikombe tisa kwa hiyo fainali hii kombe lazima litue Vingunguti”, alisema Mbwembwe.

“Kwanza mimi nina kijiji cha wachezaji achilia mbali hao waliotoka mikononi mwangu ambao kwa sasa wanamajina makubwa kwenye soka la Tanzania na duniani. Wachezaji wengine ambao wametoka mikononi mwangu nafanya kitendo cha kuwapigia simu tu waje watusaidie kwenye mechi zetu wanakuja bila tatizo”.

“Hawa ndugu zetu waliongea sana kabla ya mchezo wetu wa nusu fainali sisi tukakaa kimya tukisubiri kuoneshana kazi uwanjani. Kilichotokea wao wenyewe wanajua, sasa tunawasubiri wengine watakaokuja kati ya Kauzu FC au Friends Rangers”.

Leo utapigwa mchezo wa nusu fainali nyingine ya pili kati ya Friends Rangers dhidi ya Kauzu FC kama ulikosa mechi ya jana basi leo ‘Toroka Uje’ uwanja wa Bandari, Tandika au kama upo mikoani na mahali popote pale unaweza kuushuhudia mchezo huo kwa kupitia vituo vya Television vya Clouds TV na Azam TV kupitia channel ya Azam Sports HD.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here