Home Kitaifa MFAHAMU SAID MAKAPu, KIUNGO WA YANGA ALIYETOKA CHIMBO HADI LIGI KUU BARA

MFAHAMU SAID MAKAPu, KIUNGO WA YANGA ALIYETOKA CHIMBO HADI LIGI KUU BARA

2707
0
SHARE
Kiungo wa timu ya Yanga Said Juma Makapu
Kiungo wa timu ya Yanga Said Juma Makapu

Said Juma Makapu ni jina linalokua kwa kasi na kujizolea umaarufu mkubwa kila kukicha, huyu ni mchezaji wa mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Dar Young Africans ‘Yanga’ anayecheza nafasi ya kiungo kwenye kikosi hicho.

Makapu ni mzaliwa za Zanzibar aliyeanza soka lake kwenye klabu ya Shangani FC ya Zanzibar lakini alichaguliwa kutengeneza kikosi cha Taifa Stars Maboresho kwenye program ya kuandaa timu ya Taifa kuanzia kwa vijana. Baada ya kuonesha kiwango kikubwa alionekana na makocha na kuorodheshwa miongoni mwa vijana watakaounda kikosi cha Maboresho.

Makapu jana alipiga stori na Abubar Kisandu na kumweleza siri ya mafanikio yake kuwa ni nidhamu kwa makocha wanaomfundisha na kufuata yale yote anayoelekezwa na makocha wake, siri nyingine ya mafanikio yake ni mazoezi.

Kijana huyo mwenye miaka 20, anasema kuwa mehi ambayo hatoisahau kwenye maisha yake ya soka ni ile kati ya Yanga dhidi ya Azam FC kwani ndio ilikuwa mechi yake kubwa ya kwanza kucheza katika historia yake kwenye soka. Mechi hiyo ambayo ilikuwa ni ya kwanza kwake akiwa na Yanga ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa goli 3-1.

Makapu amewashauri wachezaji wa ligi ya Zanzibar kuwa wasikate tamaa, wajitume na kuonesha uwezo wao kwani hata wao wanaweza kucheza kuliko hata yeye (Makapu).

Akaeleza pia utofauti wa soka la Zanzibar na Tanzania bara kuwa, maslahi ya Zanzibar ni madogo ukilinganisha na bara kitu kinachopelekea wachezaji wa bara kujituma wakijua mpira ndio kazi yao lakini Zanzibar watu wanacheza kama kujifurahisha.

Kwa upande wa mafanikio Makapu amesema yapo mengi lakini hawezi kutaja kimoja baada ya kingine lakini akisisitiza kuwa yapo mafanikio yaliyotokana na soka ambayo anajivunia mpaka sasa.

Kuhusu kuoa Makapu anasema bado anajipanga kwanza kimaisha halafu baadae muda wa kufanya hivyo ukifika ataoa.

Kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa Tanzania na Afrika, Makapu pia ana ndoto za kucheza soka nje ya Afrika lakini awaahidi wana Jangwani wasubiri mambo mazuri zaidi ya yale ambayo tayari ameshayaonesha mpaka sasa.

Hapa chini nimekuwekea sauti ya Makapu wakati akipiga stori na Abubakar Kisandu, bofya hapo kusikiliza stori nzima…

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here