Home Kimataifa HUU NDIO USHAURI WA MICHAEL OWEN KWA MANCHESTER UNITED

HUU NDIO USHAURI WA MICHAEL OWEN KWA MANCHESTER UNITED

462
0
SHARE

OwenBaada ya kupoteza mechi dhidi ya Swansea kwa magoli 2-1 katika ligi kuu ya soka nchini England, mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Madrid na Manchester United pia alitoa ushauri wake kwa klabu yake ya zamani ya Manchester United.

Akiandika kupitia ukurasa wake wa twitter, Michael Owen ambaye hivi sasa ni mchambuzi wa masuala ya soka katika channel za BT Sports amesema Manchester United inamhitaji winga ya kulia kwani Juan Mata ni mchezaji wa kati na kwamba hawezi kucheza winga.

Akimtaja winga ambaye anaweza kupatikana katika siku mbili hizi za mwisho za usajili, Owen anasema anaamini pamoja na umri kusogea, lakini winga Arjen Roben anaweza kuongeza kitu kikosini hapo ili kuamsha ari ya safu ya ushambuliaji.

Kocha Loius Van Gaal amekua akimtumia Juan Mata kucheza sehemu hiyo ya winga ya kulia huku akiwa hana amshaamsha na kusababisha timu kupunguza presha katika eneo la tatu ya mwisho ya uwanja wakati timu inapokuwa inashambulia.

Aidha mkongwe Rio Ferdinand, kupitia twitter pia ameonesha masikitiko yake ya kupoteza mchezo huo kwa timu yake ya zamani, huku akiamini kuwa itajipanga upya na kurudi kuwapa raha wapenzi wake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here