Home Kitaifa SIMBA YAANGUKIA PUA ZENJI, YAKUBALI KIPIGO SAAAFI…

SIMBA YAANGUKIA PUA ZENJI, YAKUBALI KIPIGO SAAAFI…

308
0
SHARE

Simba vs URA 2Wekundu wa Msimbazi’ Simba leo imekubali kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa JKU ya Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

Mchezaji Mbaruku Chande wa JKU aliifungia goli la kwanza timu yake dakika ya 32 kipindi cha kwanza huku bao la pili likifungwa na Hamisi Said dakika ya 72 kipindi cha pili.

Katika mchezo huo, Simba imewachezesha wachezaji wake wawili wa kimataifa kutoka Mali na Senegal wanaofanya majaribio kwenye timu hiyo ili mmoja wao kama atamvutia kocha na benchi zima la ufundi asajiliwe kwa ajili ya msimu ujao.

 Baada ya kipigo hicho kocha wa Simba Dylan Kerr alimlalamikia mwamuzi wa mchezo huo kwa kitendo cha mwamuzi huyo kumkatalia kumuingiza mchezaji ambaye alishacheza akatolewa kupumzika kisha kocha huyo akataka kumuingiza tena uwanjani kwa madai kwamba walikuwa wamekubaliana kabla ya mchezo kuanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here