Home Kitaifa AZAM, MWADUI KUJIPIMA UBAVU LEO CHAMAZI

AZAM, MWADUI KUJIPIMA UBAVU LEO CHAMAZI

308
0
SHARE

KCCA-vs-Azam-4Kikosi cha Mwadui FC leo kinajitupa uwanjani kuwakabili mabingwa wa kombe la Kagame ‘wanalambalamba’ Azam FC ikiwa ni siku mbili baada ya kuikomalia timu ya Simba na kutoka sare ya bila kufungana kwenye mechi ya kirafiki iliyopigwa siku ya Jumatatu kwenye uwanja wa Taifa.

Mchezo huo wa kirafiki kati ya Azam dhidi ya Mwadui FC utapigwa kwenye uwanja wa Chamazi Complex kuanzia saa 1:00 usiku.

Afisa habari wa Azam FC Jafar Idd Maganga amethibitisha kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki huku akisema, mchezo huo utatumiwa na waalimu wa timu zote mbili (Azam FC na Mwadui FC) kuangalia vikosi vyao lakini pia wachezaji kupata changamoto kabla ya kuingia kwenye ligi.

Kabla ya mchezo huo kutakuwa na mchezo mwingine wa kirafiki kati ya Azam U20 dhidi ya timu ya Polisi ya Dar es Salaam ambao utaanza saa 10:00 jioni.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here