Home Kimataifa MAKALA : VIPIGO VYA BARCA…MCHAWI WA KWANZA ENRIQUE, WA PILI HUYU HAPA

MAKALA : VIPIGO VYA BARCA…MCHAWI WA KWANZA ENRIQUE, WA PILI HUYU HAPA

430
0
SHARE

barca

‘Nyumba mlango’ Hii ina maana mlango ukiwa mbovu hata nyumba itakuwa haijakamilika. Barcelona mwishoni mwa wiki iliruhusu magoli 4 ugenini kutoka kwa Atletco Club Bilbao, siku chache zilizopita iliruhusu magoli 4 kutoka Fc Sevilla. Kama hii haitoshi kwenye mechi za ‘Pre season’ pia waliruhusu magoli kibao. Inawezeka mabeki wanapwaya ila unapozungumzia walinzi kwenye soka unamjumuisha na Mlinda mlango. Inawezekana Golikipa katika mechi hizi naye akawa na mapungufu, leo naomba tumjadili Golikipa wa Barcelona ambaye ameruhusu magoli takribani 16 ndani ya mechi zisizozidi 10. Karibu…

Baada ya kuondoka kwa Mlinda mlango ambaye hajawahi kufungwa ‘hat-trick’ Victor Valdes na Jose Manuel Pinto, tarehe 19 may 2014 mabingwa wa ulaya, Fc Barcelona walimtangaza Marc-Andre Ter Stegen, kijana mdogo aliyekuwa na miaka 22 wakati huo. Kinda aliyezaliwa jijini Monchengladbach na mara kadhaa Wajerumani walimtaja kama mtu anayefuata nyayo za Manuel Nuer. Tangu akiwa na miaka 16 ameiwakilisha Ujerumani kwenye michuano yote ya vijana hadi alipofikisha miaka 22. Mechi zote za vijana alikuwa anaanza licha ya kuachia magoli mara kwa mara kama desturi yake.

Ter Stegen alianza vyema baada ya kutoa ‘Clean sheets’ 4 ndani ya mechi 5 za mwisho wa ligi mwaka 2011 na kuinusuru Monchengladbach kuteremka daraja. Hali hii iliwavutia Barcelona na kujikuta wanatoa €12 million na kumvuta Camp Nou huku wakiweka kipengele cha €80 million endapo atasajiliwa na timu nyingine. Kiburi hiki walikipata kutokana na wao kuamini huyu ni Manuel Neur mpya. Claudio Bravo ndiye aliyepaswa kukaa benchi ila majeruhi kabla ya msimu aliyoyapata Ter Stegen yalimfanya kucheza mechi chache tena zisizozidi 10 msimu
uliopita.

Japokuwa Joachim Low alimuita kwenye kikosi cha timu ya taifa, Stegen alidhihirisha kuwa yeye hakupaswa kuitwa baada ya kufanya madudu ya kutosha. Mechi yake ya kwanza akiwa na timu yake ya taifa aliruhusu magoli 5 pale Uswisi iliposhinda 5-3. Japokuwa alipangua penati ya Messi kwenye mechi dhidi ya Argentina, hii haikutosha kwani bado aliruhusu magoli mengine 3 kutoka kwa Argentina. Alikamilisha kapu la magoli 12 katika mechi 3 pale Marekani ilipoinyuka Ujerumani 4-3 kwenye mechi ya kirafiki mwezi June 2013. Hapo ndo utagundua kupigwa magoli mengi katika mechi chache ameanza siku nyingi.

Tarehe 27 June mwaka huu aliruhusu magoli 5 kwenye mechi 2 pale alipokuwa na timu yake taifa ya Ujerumani ya vijana chini ya miaka 21. Aliwahi kurudishiwa pasi na beki wake Benedikt Howedes pindi walipokuwa wanacheza na Marekani, huwezi kuamini alishindwa ‘ku-control’ mpira na kusababisha goli la kujifunga. Ameonekana kujisahau mara kwa mara kwa usishangae kuona anafungwa goli la mbali kama alilofungwa juzi baada ya kutoka golini.

Ni jambo la kushangaza sana kwa Mlinda mlango kama huyu aliyekuwa anatabiriwa makubwa kucheza mechi 4 na kupata ‘clean sheet’ moja pekee tena kwenye timu ya kawaida kama Poland ambayo ilikuwa inacheza Ujerumani hivyo presha ya kushambulia inakuwa ndogo. Haya ni baadhi ya mambo machache ambayo yanawapa mashaka mashabiki wa Barcelona kwani hadi sasa ametoa clean sheat zisizozidi 5 tangu apangwe kuanza kwenye
milingoti mitatu ya pale golini.

Utakumbuka magoli 3 dhidi ya Man u, 2 dhidi ya Chelsea kwenye mechi za ‘pre season’ yalichagizwa na kiwango chake cha mashaka, inawezekana majeraha kabla ya ligi msimu uliopita bado yanachangia kiwango chake. Magoli 4 aliyoruhusu pale Tbilisi dhidi ya Sevilla yalipaswa kumpa changamoto ya kufanya vyema kwenye milingoti mitatu ila cha kushangaza Ijumaa aligeuka pazia tena kwa kuruhusu magoli 4 ugenini. Japokuwa aliaminiwa kwa kucheza fainali ya Uefa pale Ujerumani na ile kombe la mfalme, bado alishindwa kutoa ‘Clean-sheat’ kwenye mechi hizo.

Kutokana na takwimu hizi ni wazi kuwa baada ya Enrique kukosa mbinu mbadala za kuisuka safu yake ya ulinzi, ‘goalkeeper’ huyu pia ameonekana kikwazo hasa tabia yake ya kushindwa kuzungumza na mabeki
wake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here