Home Kimataifa RAIS WA URUSI AMSAFISHA BLATTER

RAIS WA URUSI AMSAFISHA BLATTER

398
0
SHARE
Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter anastahili kwa heshima zote kupewa tuzo ya heshima ya Nobel kwa mchango wake mkubwa katika soka.
Blatter alikutana na Putin siku ya Jumamosi huko St. Petersburg wakati akitangaza nia thabiti ya FIFA katika kuisapoti Urusi kuandaa kombe la dunia mwaka 2018.
Na Putin sasa ambaye amekuwa akizungumza kuhusu tuhuma za rushwa zinazoelekeza kwa Blatter amesema kwamba kwa upande wake haoni kama tuhuma hizo zina ukweli wowote.
“Sote kwa pamoja tunajua hali inayomkabili Blatter kwa sasa. Sitaki kwenda ndani zaidi ila sitaki pia kuamini kuhusu tuhuma hizi za rushwa zinazoelekezwa kwake”. alinukuliwa na RTS.
“Nadhani watu wanampenda Blatter au mkuu wa taasisi kubwa kabisa ya michezo, au michezo ya Olimpiki, anahitaji heshima maalum. Kama kuna mwingine yeyote anayehitaji tuzo hii ya Nobel basi ni watu hao.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here