Home Kimataifa VAN GAAL AMHAKIKISHIA WAYNE ROONEY KITU ROHO INAPENDA

VAN GAAL AMHAKIKISHIA WAYNE ROONEY KITU ROHO INAPENDA

403
0
SHARE
2A9B3DD300000578-3167430-image-a-26_1437344717226
Louis van Gaal amemwambia Wayne Rooney kwamba ndiye atakuwa mshambuliaji wa kati wa kutegemewa msimu ujao..
Baada ya msimu uliopita kuchezeshwa nafasi nyingi uwanjani kutokana na mahitaji ya United ikiwemo safu ya kiungo, nahodha huyo wa Man United amehakikishiwa kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati.
Rooney has been told he will line up there when United's season begins against Tottenham on August 8 
United inaweza kununua mshambuliaji mwingine kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili ili kuziba mapengo ya Radamel Falcao na Robin van Persie ambao wametimka.
Hata hivyo inafahamika kwamba Van Gaal na Mkurugenzi mkuu wa United, Ed Woodward hawana hofu kabisa licha ya washambuliaji hao kuondoka.
Wanaamini Rooney ataweza kung’ara na kufunga magoli kama atatumika vizuri msimu ujao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here