Home Kimataifa MASWALI 5 NA MAJIBU KUTOKA KWA THIERRY HENRY KUHUSU FAINALI YA UEFA...

MASWALI 5 NA MAJIBU KUTOKA KWA THIERRY HENRY KUHUSU FAINALI YA UEFA 2015

402
0
SHARE

TT

Swali: Fainali ya UEFA itakua historia kubwa na kati ya Barcelona au Jeventus watachukua kombe. Wewe umewai kufanikiwa mwaka 2009, unaweza kusema chochote juu ya usiku wa fainali ya UEFA.
TH: Ni ngumu sana kufanikiwa kushinda kombe, inatakiwa kuwa na umoja, uwezo na Imani ndani yenu pia kuwa hamu ya kushinda pamoja na kujitolea. Siamini juu ya bahati, chochote unachokifanya vizuri ni kwasababu una uwezo wa kukifanya vizuri. Kuna wakati utapata usaidizi mzuri kati ya wenzako kwenye timu lakini sio swala la bahati.

Swali: Unaionaje Barcelona hii na yenu?
TH: Sipendi kufananisha timu lakini naamini hivi sasa Barcelona wana team nzuri sana.

Swali: Timu yenu na hii ya sasa hivi unadhani ipi ina best three players mbele
TH: Nadhani hawa wa sasa hivi wameshinda magoli mengi, lakini ishu sio tu kufunga magoli mengi. Upande wangu ni zaidi sio magoli tu, unaweza kurudi nyuma kwenye historia ukaona wachezaji wazuri zaidi waliofanya vizuri pale mbele. Kinachotakiwa ni kuwa na balance nzuri pale mbele, nadhani hawa wa sasa wanayo hiyo balance.

Swali: Unadhani Juventus inaweza kuzuida mapacha watu pale mbele?
TH: Juventus ipo vizuri sana kuanzia Alvaro Morato, Carlos Tevez na Paul Pogba. Kuna Claudio Marchisio na pia tusimsahau Adrea Pirlo. Pia tunajua jinsi gani Juve walivyowazuri pale nyuma na pia wanaweza kukaa na mpira pia. Lakini kwenye hii fainali hawawezi kukaa na mpira zaidi ya Barcelona japokuwa uwezo uwezo wa kuzuia wanao.  Kwangu mimi timu yoyote inayotaka kuzuia Barcelona inabidi wazuie timu nzima na sio mchezaji mmoja.

Swali: Unaamini Juventus wanaweza kubadilisha mawazo ya watu na kuwafunga Messi na wenzake?
TH: Chochote kinaweza kutokea kwenye fainali. Nakumbuka Juve Vs Madrid mwaka 98, kila mtu alijua matokea jinsi yatakavyokua lakini mambo yakawa tofauti. Fainali haitabiliki.

Swali: Unatua umekaa kwenye kiti unaangalia mechi kupitia Sky Sports lakini je utajiskia wivu kama hauchezi ile mechi?
TH: Nimecheza fainali nakushinda lakini nimecheza na kufungwa pia nikiwa na Arsenal. Lakini ningejiskia vizuri kucheza fainali ya mwaka huu pia.

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here