Home Kimataifa 19 MAY: PITIA HIZI HIGHLIGHTS ZA MAGAZETI YA MICHEZO KUTOKA ULAYA NA...

19 MAY: PITIA HIZI HIGHLIGHTS ZA MAGAZETI YA MICHEZO KUTOKA ULAYA NA TANZANIA

615
0
SHARE

gazeri

ISHU YA KOCHA NI PASUA KICHWA KWA SIMBA

Mchakato wa kumpata mrithi wa nafasi ya aliyekua kocha wa timu ya simba mserbia goran kopunivic ni swala linaloumiza kichwa uongozi wa yanga. Akizungumza na gazeti la nipashe rais wa simba evans aveva amesema kwamba bado viongozi wanaendelea na mchakato wa kumpata kocha mpya lakini aliweka wazi kwamba mchakato huo unawaweka kwenye wakati mgumu kutokana na vipengele ambavyo wanakutana navyo kwa makocha wanaowataka. Nipashe michezo limeandika

HAKUNA MAPINDUZI NDANI YA YANGA

Uongozi wa Yanga umesema hauko tayari kuona mapinduzi yananafanyika ndani ya klabu hiyo kutokana na kikundi cha watu wachache wanaotaka madaraka.Pia ametangaza kuwa  Francis Kaswahili kuwa sio mwanachama wa klabu hiyo. Habari kutoka Nipashe Michezo.

 

MTANZANIA AFANYA MAJARIBIO NA TIMU YA SERIA A

Mshambuliaji Haji Ungando ametua katika timu ya Atlanta inayoshiriki ligi kuu ya nchini Italy “Serie A” kufanya majiribio ya siku 10 baada ya timu hiyo kuvutiwa nae.

Kinda huyo aliwavutia scouts wa Atlanta akitokea kwenye kituo cha kukuzia vipaji Jaki Sports Academy na hivi sasa anaendelea kuangaliwa na makocha wa timu hiyo. Limeandika Mtanzania Michezo

 

MAJIMAJI KUSAJILI WAWILI KIMATAIFA

Uongozi wa timu ya Majimaji unatarajiwa kusajili wachezaji wawili wa kimataifa ili kuimarisha kikosi chake kitakachoshiriki msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom.

Akizungumza na Mtanzania Michezo kocha wa Majimaji Hassan Bainyai alisema wachezaji hao watatoka nchi za jirani Malawi na Zambia.

 

LIGI YA KICK BOXING YAZINDULIWA

Ligi ya mabingwa ya michezo ya kick boxing imezinduliwa rasmi juzi kwa michezo miwili kufanyika huku wapiganaji zaidi ya 30 wanashiriki. Katika ufunguzi wa ligi hiyo uliwakutanisha Hamisi Mwanyiko kutoka Tanga dhidi ya Ramadhani Mshana na Mrisho Ally na Ally Chande. Mratibu wa ligi hiyo Kaseba alisema ligi hiyo ilisimama kwa muda lakini imeanza rasmi. Habari na Majira Michezo.

JAMES MILNER KUPOTEZEA OFA YA LIVERPOOL

Midfielder James Milner mwenye miaka 29 anategemewa kuopotezea ofa ya Liverpool ya kulipwa pound 165,000 kwa wiki ili kujunga na Arsenal. Mchezaji huyo ni raia wa England na habari imeandikwa na gazeti la Daily Star

GARY NEVILLE AIPA USHARI MAN UNITED

Mchezaji wa zamani wa Man United Gary Neville amesema club yake imtumia kipa David De Gea kwenye mabadilishano ya kumsaini mchezaji Gareth Bale mweye miaka 25 ambae yupo kwenye wakati mgumu ndani ya Real Madrid na mashabiki wao. Limeandika Gazeti la The Sun

REAL MADRID WANAJIPANGA KUTOA UAMUZI KUHUSU CARLO ANCELOTTI

Real Madrid inajipanga kutoa taarifa kuhusu ishu ya kocha kwenye timu yao. Kitakacho zungumziwa hasa ni kuhusu Carlo Ancelloti kuendelea kuifundisha timu hiyo au la. Japokua Carlo mwenyewe anapanga kuendelea kufundisha timu hiyo.

 

LIVERPOOL WANAMTAKA MCHEZAJI HUYU

Baada ya kuondokewa na legend wao Steven Gerrard , Liverpool inaendelea kufanya harakati za kukiimarisha kikosi chao. Hivi sasa Liverpool inafanya harakati za kumsajili mchezaji kutoka Bosnia Edin Dzeko. Habari na gazeti la Mail.

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here