Home Kitaifa Dakika 45 za Kwanza Yanga 1-1 Azam, Taifa

Dakika 45 za Kwanza Yanga 1-1 Azam, Taifa

796
1
SHARE

ngassa-azam (1)Na. Richard Bakana, Dar es salaam.

Dakika 45 za kwanza za Mchezo wa Ligi kuu kati ya Yanga SC pamoja na Azam FC unaopigwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam zimemalizika huku Vinara hao wa VPL wakiwa wamefungana bao 1-1 yakifungwa na Andrey Coutinho wa Yanga pamoja na Bryson wa Azam.

ILIKUA HIVI DAKIKA 45 ZA MWANZO

Dakiakya 2 azam wanapata kona ya kwanza lakini wanashindwa kuifanyia kazi

Tambwe anaikosesha bao Yanga dakika ya 3 baada ya kuingiza krosi ambayo inakosa macho na kuokolewa na mabeki wa Azam.

Azam wanakosa bao baada ya Brian Majwega kupiga krosi lakini Tchetche anachelewa na kuokolewa na mabrki wa Yanga ikiwa ni dakika ya 6.

Dakia ya 7 Azam FC wanakosa bao baada ya Kipre Tchetche kupaisha mpira juu akiwa na kipa baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Himid Mao.

Dakika ya 12 Yanga wanapata bao la kwanza baada ya Andry Coutinho kupiga mpira wa Adhabu na kuingia moja kwa moja.coutinho

Dakika ya 14 Azam wanasawazisha bao kupitia kwa Bryson Raphael baada ya Mwaikimba kukosa bao akiwa pekee yeye na mpira.

Dany Mrwanda anakosa bao kunako dakika ya 21 baada ya kupiga shuti kali na kutoka nje kidogo ya lango la Azam FC.

Dakika ya 27 Yanga wanapata faulo baada ya Shomari Kapombe kumfanyia madhambi Coutinho ambapo mpira ulipigwa na kuishia kwa mabeki wa Azam ,

Azam FC wanakosa bao katika dakika ya 28 baada ya Kipre Tchetche kupiga shuti ambalo lilimbabatiza Deogratius Munishi Dida na kutoka nje.

Kipre Tchetche anakosa bao baada ya kupiga krosi ambayo mpira uligonga mwamba wa juu na kurudi Ndani ikiwa ni dakika ya 34.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here