Home Kitaifa Prisons yagoma kushuka ikiifumua Mgambo

Prisons yagoma kushuka ikiifumua Mgambo

507
0
SHARE
cb4a0-1375766_581274061909694_1850204431_n-Copy
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
‘Kocha mkuu wa Prisons, Mbwana Makata, ameahidi Prisons haitashuka daraja msimu huu.’
KIKOSI cha Tanzania Prisons kimeendelea kuinyanyasa Mgambo Shooting Stars jijini Mbeya baada ya leo kuichapa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini humo.
Kwa ushindi huo, Prisons ambayo iko hatarini kuporomoka daraja msimu huu baada ya kunusurika mwaka jana ikilazimika kushinda mechi ya mwisho dhidi ya Ashanti United FC mjini Mororogo, kimeongeza pointi tatu, hivyo kufikisha pointi 25 baada ya mechi 24 sawa na Ndanda FC iliyopo nafasi ya pili kutoka mkiani.
Hata hivyo, timu hiyo ya Jeshi la Magereza nchini badso inaendelea kukaa mkiani mwa msimamo wa VPL na inahitaji kushinda mechi mbili zinazofuata ili kuukwepa mstari wa kushuka daraja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here